Pata taarifa kuu

Serikali ya Tanzania imetakiwa kuwaachia wanaozuiliwa kwa tuhuma za uchochezi

Mamlaka nchini Tanzania ni lazima ziwaachie haraka na bila masharti, mwanasiasa Wilbrodad Silaha, wakili Boniface Mwabukusu na mwanaharakati Mdude Nyagali, ambao wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi, imesema taarifa ya shirika la kimataifa la kutetea haki za bindamu Amnesty International.

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Raia hawa walikuwa mstari wa mbele kuikosoa Serikali na kupinga makubaliano ya kiuwekezaji kwenye bandari kati ya Tanzania na Dubai, wakisema mkataba huo hauna maslahi kwa taifa.

Taarifa ya polisi ilitolewa baada ya uvumi kuwa walikamatwa na kupelekwa kusikojulikana, sasa polisi ikithibitisha kumshikiliwa wakili Boniface Mwabukusi aliyefungua kesi hivi karibuni kupinga mkataba wa makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai.

Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema.

“Watu wanakamatwa kwa sababu serikali ya rais Samia Suluhu Hassan inaogopa kelele za wanachi kwa sababu ya haya makubaliano iliyofanya na Dubai.” alisema Tundu Lisu.

Tangu bunge lipitishe makubaliano hayo, kumeibuka mjadala mkali ambapo wapo wanaounga mkono na wengine wakipinga, huku wanaharakati wa haki, wakiituhumu Serikali kujarubu kuwanyamazisha wakosoaji wake.

Polisi nchini Tanzania, wiki hii ilithibitisha kuendelea kumshikilia wakili mmoja na mwanasiasa wa upinzani kwa kile imesema wanatuhumiwa kwa uchochezi na kupanga kuandaa maandamano ya kitaifa yanayolenga kuiangusha Serikali.

Wakili Philip Mwakilima anayewawakilisha wawili hao, akizungumza na shirika la habari la Reuters, alisema anatarajia kukutana na wanaozuiliwa na kwamba mashtaka dhidi yao yamechochewa kisiasa na yametengenezwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.