Pata taarifa kuu

Tanzania: Watuhumiwa wa kupanga kuandaa maandamano wazuiliwa

Nairobi – Polisi nchini Tanzania, imethibitisha kuendelea kumshikilia wakili mmoja na mwanasiasa wa upinzani kwa kile imesema wanatuhumiwa kwa uchochezi na kupanga kuandaa maandamano ya kitaifa yanayolenga kuiangusha Serikali.

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya polisi ilitolewa baada ya uvumi kuwa walikamatwa na kupelekwa kusikojulikana, sasa polisi ikithibitisha kumshikiliwa wakili Boniface Mwabukusi aliyefungua kesi hivi karibuni kupinga mkataba wa makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai.

Aidha polisi pia inamshikiliwa mwanasiasa wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, Mpaluka Nyagali maarufu kama mdude, iliongeza tarifa ya msemaji wa jeshi la polisi David Misime.

Wakili Philip Mwakilima anayewawakilisha wawili hao, akizungumza na shirika la habari la Reuters, amesema anatarajia kukutana não na kwamba mashtaka dhidi yao yamechochewa kisiasa na yametengenezwa.

Kukamatwa kwao kumekuja baada ya Ijumaa ya wiki iliyopita, mkuu wa jeshi la polisi nchini humo, Camilius Wambura, kudai kuwa wanapanga kuwachukulia hatua watu wanaopanga kuchochea vurugu ikiwemo kuipindua Serikali y arais Samia Suluhusu Hassan kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025, akisema vitendo hivyo ni sawa na uhaini.

Haya yakijiri, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, limesema watu 22 wamekamatwa tangu mwezi Juni kwa kulikosoa bunge la nchi hiyo kupitisha mkataba ambao umezua mjadala mkali, huku msemaji wa Serikali Gerson Msigwa, akikanusha madai kuwa Serikali inataka kunyamazisha sauti za upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.