Pata taarifa kuu

Niger: Uongozi wa kijeshi unasema hautatishwa na shinikizo za Kimataifa

Nairobi – Kiongozi wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani  katika hotuba kwa taifa usiku wa kuamkia leo, amesema jeshi halitatishwa na shinikizo za Kimataifa kukabidhi kurejesha madaraka kwa rais Mohamed Bazoum, lakini pia kulaani vikwazo ilizowekewa na ECOWAS.

Kiongozi wa mapinduzi ya Niger ametangaza kuwa hatakubali kushinikizwa kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa Mohamed Bazoum
Kiongozi wa mapinduzi ya Niger ametangaza kuwa hatakubali kushinikizwa kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa Mohamed Bazoum © RTN
Matangazo ya kibiashara

Wakati Jenerali Tchiani  akitoa kauli hiyo, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, imetuma ujumbe kwenda kuzungumza na uongozi wa kijeshi nchini Niger, huku wakuu wa Majeshi kutoka nchi hizo waliokutana jana jijini Abuja, wakisema matumizi ya nguvu itakuwa ni hatua ya mwisho.

Ili kuendelea kuliwekea jeshi shinikizo, Nigeria imekata umeme unaokwenda nchini Niger, huku Ufaransa ikituma ndege yake ya tano kuwaondoa raia wake.

“Vikwazo hivi ni vya kijinga na vya kidhalimu, vinalenga kudhalilisha majeshi ya ulinzi na usalama ya Niger, taifa la Niger na watu wake kwa lengo na kufanya nchi isitawalike kabisa.” alisema Jenerali Abdourahamane.

00:38

Jenerali Abdourahamane, Kiongozi wa kijeshi nchini Niger

Kiongozi wa mapinduzi ya Niger ametangaza kuwa hatakubali kushinikizwa kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa Mohamed Bazoum, akikashifu vikwazo vilivyowekwa na viongozi wa Afrika Magharibi kuwa ni "kinyume cha sheria" na "kinyama" na kuwataka wananchi wake kuwa tayari kutetea taifa lao.

Maoni ya Jenerali Abdourahamane Tchiani, yaliyotolewa katika hotuba ya televisheni siku ya Jumatano, yalikuja wakati wakuu wa ulinzi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) walipokutana katika nchi jirani ya Nigeria kujadili mgogoro wa Niger.

Uongozi wa ECOWAS umetaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia  nchini Niger
Uongozi wa ECOWAS umetaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Niger © AFP/Kola Sulaimon

Umoja wa kikanda umeiwekea Niger vikwazo vikali vya kiuchumi na kutishia kutumia nguvu ikiwa urais wa Bazoum hautarejeshwa ifikapo Agosti 6. Pia umetuma ujumbe kwenda Niger - unaoongozwa na kiongozi wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar - kufanya mazungumzo na wanajeshi walionyakua mamlaka. .

Siku ya Jumatano, mmoja wa viongozi wa mapinduzi ya Niger, Jenerali Salifou Mody, aliwasili na ujumbe wake katika mji mkuu wa Mali Bamako.

Katika mahojiano yaliyotangazwa na televisheni ya taifa ya Mali, alisisitiza haja ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.