Pata taarifa kuu

IMF yaipa Burundi mkopo wa dola milioni 271, ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mingi

Benki Kuu ya Burundi imetangaza kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), siku mbili zilizopita, mkopo wa dola milioni 271 kwa zaidi ya miaka 3, kwa nia ya "kuunga mkono mageuzi ya kiuchumi" katika nchi hii, iliyoainishwa kama maskini duniani kulingana na Benki ya Dunia.

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi umetolewa kwa wakati unaofaa, kutokana na hali mbaya ya kiuchumi ya nchi. Uamuzi huu ulikuwa unasubiriwa kwa hamu huko Gitega, mji mkuu wa Burundi, kwa miezi mitatu. Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) hatimaye iliidhinisha Jumatatu hii, Julai 17 makubaliano yaliyohitimishwa kati ya pande hizo mbili mwezi Aprili, ambayo ni ya kwanza ya aina yake tangu mgogoro wa 2015 nchini Burundi.

Mwishowe, IMF itaikopesha Burundi kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kusaidia mageuzi ya kiuchumi ambayo inapaswa kufanya. Gitega imejitolea hasa kuongeza mapato yake ya ndani, kuunganisha soko rasmi na sambamba la kubadilishana fedha baada ya kuwa tayari imepunguza thamani ya sarafu yake kwa 38%, kufanya soko hili kuwa huria, na kupambana na rushwa.

IMF imejitolea kutoa mara moja sehemu ya msaada huu, dola milioni 62.6 ambazo zinapaswa kuwekwa kwenye hazina ya serikali leo, kulingana na vyanzo vyetu, anaripoti mwandishi wetu wa habari Esdras Ndikumana.

Nchi iliyo hatarini kudorora kiuchumi

Ukosefu wa fedha za kigeni, uhaba mkubwa wa mafuta, sukari na hata vinywaji... Furaha iliyoje kwa nchi hii iliyoainishwa kama maskini zaidi duniani na Benki ya Dunia, na ambayo ilikuwa ikikaribia kudorora kiuchumi, amebaini mmoja wa wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini Burundi. Hata hivyo, mchambuzi huyu anabaini kuwa hilo halitatosha kutokana na changamoto nyingi zinazoikabili nchi hii, na hasa ufisadi unaokumba mamlaka.

Lakini "juu ya yote ni ishara iliyotumwa kwa wafadhili wote wa Burundi ambao walikuwa wakisubiri mkataba huu kuanza tena misaada yao", amebainisha afisa mmoja wa IMF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.