Pata taarifa kuu

Burundi imepokea mkopo unaofikia dola za Marekani milioni 261 kutoka kwa IMF

NAIROBI – Nchi ya Burundi, imepokea mkopo unaofikia dola za Marekani milioni 261 kutoka kwa shirika la fedha duniani, IMF, fedha ambazo zinatarajia kupiga jeki juhudi za kufufua uchumi wa taifa hilo.

Nembo ya shirika la fedha duniani
Nembo ya shirika la fedha duniani REUTERS - Johannes Christo
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni baada ya mikutano kadhaa kati ya wawakilishi wa IMF walioongozwa na mkuu wa shirika hilo nchini Burundi, Mame Astou Diouf, ambaye alitembelea taifa hilo mwezi Februari.

Katika taarifa yake, IMF imesema kwa kushirikiana na mamlaka za Burundi, wamefikia makubaliano ya mkopo wa miezi 40 ambapo nchi hiyo itapata kiasi cha dola za Marekani milioni 261.1, chini ya mpango wa kuzisaidia nchi zenye kipato cha chini.

Hii ni mara ya kwanza kwa mpango kama huu kuchukuliwa kwaajili ya nchi ya Burundi tangu mwaka 2015, imesema taarifa ya IMF, ambapo imeongeza kuwa, mkopo huu utasaidia serikali kutekeleza sera za kiuchumi ikiwemo ubanaji matumizi na kuifanya iwe na uwezo endelevu wa ulipaji madeni na yanayostahimilika.

Uchumi wa Burundi umetatizika kwa kuchangiwa na masuala kadhaa, ikiwemo athari hasi zilizotokana na mlipuko wa Uviko 19 na kutokuwepo kwa urari wa kibiashara.

Aidha uhaba wa mvua ulioshuhudiwa tangu mwaka uliopita, kutopatikana kwa wakati kwa mbolea kulikochochewa na kupanda kwa bei na uhaba wa fedha za kigeni katika uagizaji wa bidhaa nje ya nchi na pia vuta ya Ukraine na uzalishaji hafifu wa ndani ya nchi kulitatiza pakubwa shughuli za uzalishaji wa kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.