Pata taarifa kuu

Dunia kuadhimisha siku ya kimataifa ya Kiswahili wiki hii

Nairobi – Siku ya Ijumaa, dunia itaadhimisha siku ya Kimataifa ya Kiswahili. RFI Kiswahili nasi pia kila siku tunachangia katika ukuaji wa lugha hii. Kila siku kuelekea maadhimisho hayo tutakuletea ripoti na uchambuzi kuhusu maendeleo ya Kiswahili.

RFI Kiswahili ni miongoni mwa redio zinazopeperusha matangazo yake kwa lugha ya kiswahili
RFI Kiswahili ni miongoni mwa redio zinazopeperusha matangazo yake kwa lugha ya kiswahili © Studio graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Jijini Mombasa Pwani ya Kenya, kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise na makumbusho ya taifa kwa ushirikiano wameandaa matukio mbalimbali kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani.

Sherehe hii ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 7 hadi 9 mwezi huu huko Mombasa inalenga kuvutia watali wa ndani  na wale kutoka mataifa za kigeni.

Khalid Kitito ni mratibu wa taasisi ya mafunzo ya kitamaduni ya shirika la makumbusho la kitaifa nchini Kenya. Anazungumzia umuhimu wa siku ya lugha ya Kiswahili.

Siku hii inamaanisha kwamba lugha ya Kiswahili itasambaa na kuenea zaidi ulimwenguni,baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kufunza watoto wao lugha ya Kiswahili inayolenga kuwauganisha waafrika wote.” amesemaKhalid Kitito.

00:18

Khalid Kitito ni mratibu wa taasisi ya mafunzo ya kitamaduni ya shirika la makumbusho la kitaifa nchini Kenya

Kituo cha utamaduni cha Ufaransa, Alliance Française, jijini Mombasa kinashirikiana na shirika la makumbusho la kitaifa nchini kufanikisha siku hii kwa kutumia ukumbi wake kuonyesha picha zilizo na maudhui ya kitamaduni. Lucas Malcor ni mkurugenzu wa kituo hicho.

“Tunafundisha Kifaransa na Kiswahili pia. Ni Muhimu sana kuelewa utamaduni ya kiafrika, tumefurahi kushirkiana na wadau tofauti ikiwemo ubalozi wa Ufaransa. ”amesema Lucas Malcor.

00:16

Lucas Malcor ni mkurugenzu wa kituo hicho

Najeeb Bhalo ni mmoja wa wapiga picha anayenuia kuonyesha picha alizozipiga maeneo mbalimbali Pwani ya Kenya.

“Nimewazia ni vizuri kuonyesha ile hali halisi ya utamaduni wetu kuonyesha ulivyo hususan kwa wageni. ”alisemaNajeeb Bhalo.

00:08

Najeeb Bhalo ni mmoja wa wapiga picha

Lugha ya Kiswahili inazungumziwa na watu zaidi ya Milioni 200 kote duniani.

Diana Wanyonyi Mombasa RFI Kiswahili .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.