Pata taarifa kuu

Urusi kuendelea na mazungumzo kuhusu amani na viongozi wa Afrika

NAIROBI – Kremlin inasema itaendelea na mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa bara Afrika wanaotafuta muafaka wa kumaliza vita vinavyoendelea nchini Ukraine wakati wa mkutano kuhusu Afrika na Urusi utakaofanyika mwezi ujao.

Rais wa Urusi Vladimir Putin kuendeleza mazungumzo na viongozi wa Afrika kuhusu amani nchini Ukraine
Rais wa Urusi Vladimir Putin kuendeleza mazungumzo na viongozi wa Afrika kuhusu amani nchini Ukraine AFP - PAVEL BEDNYAKOV
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi, Rais Vladimir Putin aliwapa wajumbe waliomtembelea mjini St Petersburg orodha mambo anayoaamini kuwa mengi ya mapendekezo yao yakuwa ya kimsingi.

Rais wa Afrika Kusini ni mshirika wa karibu wa rais wa Urusi
Rais wa Afrika Kusini ni mshirika wa karibu wa rais wa Urusi via REUTERS - HOST PHOTO AGENCY RIA NOVOSTI

Kundi la viongozi wa Afrika siku ya Ijumaa lilikutana na Zelenskyy nchini Ukraine, ambapo alisema mazungumzo ya amani yataanza pale tu Moscow itakapoondoa wanajeshi wake katika orodha yake.

Haya yanajiri wakati huu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akieleza kuwa China imetoa ahadi mpya ya kutopeleka silaha nchini Urusi kupigana nchini Ukraine na kuitaka serikali ya China kuwa makini kuhusu uwezekano kwamba makampuni ya China yanaweza kuipatia Urusi teknolojia.

"Sisi na nchi zingine - tumepokea uhakikisho kutoka kwa China kwamba haitoi na haitatoa msaada usiofaa kwa Urusi kwa matumizi nchini Ukraine," Blinken aliwaambia waandishi wa habari baada ya siku mbili za mazungumzo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amefanya kikao na rais wa China  Xi Jinping
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amefanya kikao na rais wa China Xi Jinping REUTERS - LEAH MILLIS

Xi Jinping wa China alipongeza mazungumzo hayo na Blinken siku ya Jumatatu katika safari iliyofuatiliwa kwa karibu ili kuhakikisha mizozo ya mataifa yenye nguvu zaidi hayatumbukii kwenye migogoro.

Haya yanajiri wakati huu pia Ukraine ikisema kuwa imechukua tena vijiji vinne vilivyokuwa vinakaliwa na Urusi katika muda wa wiki mbili zilizopita wakati huu mashambulio yakiendelea.

Aidha rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine anasema alizungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kuhusu mahitaji ya ulinzi ya Kyiv na ushirikiano zaidi kati ya nchi hizo mbili.

Kupitia kwenye ukurasa wa twitter, Zelenskyy aliandika: "Nilipigiwa simu na Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak. Tulijadili mahitaji ya ulinzi ya Ukraine na ushirikiano wetu zaidi ili kupanua uwezo wa Ukraine kwenye uwanja wa vita, hasa kupitia silaha za masafa marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.