Pata taarifa kuu

Tanzania: Viongozi wa kanisa wakamatwa na polisi kwa kuwazuiliwa wagonjwa

NAIROBI – Mamlaka nchini Tanzania imewakamata viongozi wawili wa kanisa kwa madai ya kuwazuilia makumi ya wagonjwa nchini humo wakiahidi kuwaponya kwa maombi na mitishamba ya kienyeji.

Watu hao walikuwa wamezuiliwa katika vyumba vya matope wahubiri wao wakiwaeleza kuwa watawaombea uponyonyaji
Watu hao walikuwa wamezuiliwa katika vyumba vya matope wahubiri wao wakiwaeleza kuwa watawaombea uponyonyaji © Mark Pellegrini/GFDL
Matangazo ya kibiashara

Watu hao zaidi ya mia moja walikuwa wamehifadhiwa katika wodi za kimila (vibanda vya kuezekwa kwa udongo na vitanda vya matofali) vilivyojengwa kuzunguka kanisa hilo katika kijiji cha Nyamhinza, wilayani Misungwi, Mkoa wa Kaskazini-Magharibi mwa Mwanza - bila kupokea matibabu wala chakula.

Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya watu hao ambao wamekuwa kwenye eneo hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja,  walitakiwa kujitafutia chakula hadi pale watakapopona.

Walipatikana baada ya wananchi kutoa taarifa kwa polisi kuwa baadhi ya watu wanafariki dunia baada ya kutoka hospitalini akiwemo mwanamke aliyejiunga na kanisa hilo mara baada ya kujifungua watoto mapacha.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, polisi waliwarudisha wagonjwa hospitalini kwa matibabu. Sasa wanachunguza iwapo kulikuwepo na vifo na iwapo miili ya waliofariki walizikiwa karibu na eneo hilo.

Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa uchunguzi wa awali haukuonyesha kulikuwa na watu waliozikwa kwenye eneo husika  lakini wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu.

Alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao, viongozi wa kanisa hilo William Masum na mkewe Kabula Lushika, akisema hawakuwa na vibali vya kuendesha ibada na maombi, wala kutoa huduma za tiba asilia. Hawajatoa maoni yao kuhusu tuhuma hizo.

“Sasa tunafanya uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa, wakati huo huo naomba wenyeji wenye taarifa za siri ambazo zitasaidia upelelezi kujitokeza kuzungumza na polisi,’’ alisema.

Kanisa hilo linasemekana kuwa limekuwa likifanya kazi kwa takriban miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.