Pata taarifa kuu

Victoria Kimani arejea tena na kibao chake kipya "How I Do"

NAIROBI – Baada ya kipindi cha miaka mitano, msani wa Kenya, Victoria Kimani, amerejea tena katika ulingo wa Muziki na kibao chake kipya kilichopewa jina la How I Do katika albamu yake ya tano.

Msani wa Kenya Victoria Kimani
Msani wa Kenya Victoria Kimani © Victoria Kimani - Twitter
Matangazo ya kibiashara

Victoria Kimani ni Msanii wa Kimataifa mwenye asili ya Kenya amabye Muziki wake ni mchanganyiko wa sauti ambazo zimekuwa zikimvutia katika safari zake zote.

Mwimbaji-Mwandishi wa Nyimbo aliyeshinda tuzo ametoa albamu 4 na akashirikiana na wasanii wengi wa Afrobeat kimataifa na kote duniani.

Msani wa Kenya Victoria Kimani
Msani wa Kenya Victoria Kimani © Victoria Kimani - Twitter

Balozi wa kwanza kabisa Afrika Mashariki wa Maybelline NY alikuwa miongoni mwa wasanii wachache waliochaguliwa kutumbuiza kwenye jukwaa kubwa la Coke Studio na Coca cola kwa miaka miwili mfululizo.

Victoria Kimani pia alihusika katika Kampeni ya Bono ya One kwa muda wa miaka miwili akiwa miongoni mwa wanawake na Wasichana kote barani Afrika na kukuza Kilimo kwa ushirikiano na wasanii wengine bora kutoka barani Afrika.

Msani wa Kenya Victoria Kimani
Msani wa Kenya Victoria Kimani © Victoria Kimani - Twitter

Victoria Kimani anasalia kuwa jina maarufu katika ulingo wa muziki wa Afro-Pop. Tutakuwa na msani huyo kwenye Makala yetu ya Niko Base Jumamosi ya wiki hii ambapo utasikiliza vibao vyake vipya pamoja na vile vilivyovuma katika ulimwengu wa sanaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.