Pata taarifa kuu

Kenya: Wavuvi wa dagaa katika kaunti ya Migori walalamikia kushuka kwa mapato yao

NAIROBI – Wavuvi wa dagaa katika eneo la Miuru Bay katika kaunti ya Migori nchini Kenya wanasema, mapato yao ya kiuchumi yameshuka kwa kiasi kikubwa, kufuatia hatua ya serikali ya Tanzania, kuzuia shughuli za uvuvi wa mara kwa mara katika Ziwa Victoria, ili kuruhusu dagaa kuongezeka zaidi.

Wavuvi wa dagaa katika kaunti ya Migori nchini Kenya walalamikia kushuka kwa mapato yao
Wavuvi wa dagaa katika kaunti ya Migori nchini Kenya walalamikia kushuka kwa mapato yao © RFI/Laura-Angela Bagnetto
Matangazo ya kibiashara

Kila Kunapopambazuka katika ufuo wa kibro wavuvi wanaanza shughuli zao wakiwa na matumaini kuwa wapata dagaa kwa wingi ili kuinua uchumi wao. 

Wavuvi katika eneo hili, huvuka mpaka maji yaliyo upande wa Tanzania, ili kupata dagaa, lakini kwa sasa ni vigumu. 

Tonny Juma Ogwari ni mwenyekiti wa wavuvi katika eneo hilo. 

“Kuna wakati wanafunga ziwa….tukienda tunashika na fine yao ni laki moja….hapa tunategema uvuvi, shamba zetu ni kidogo.” alieleza  Tonny Juma Ogwari ni mwenyekiti wa wavuvi katika eneo hilo.

00:12

Tonny Juma Ogwari ni mwenyekiti wa wavuvi Miuru Bay

Pamela Aoko amekuwa akitegema biashara ya dagaa tangu utotoni mwake, anasema hali ni mbaya. 

“Natuma dagaa kisumu Mombasa, tunaumia, hatuna pesa, watoto wamefukuzwa shule.” alisema  Pamela Aoko.

00:07

Pamela Aoko muuzaji wa dagaa

James Aira, anawataka wavuvi wenzake kubadilisha mbinu. 

“Wavuvi ni wengi sasa tuache kuvua  dagaa na tuvue samaki wengine.” alieleza  James Aira.

00:07

James Aira, Mvuvi

Mapema mwezi huu, serikali ya Tanzania ilitangaza utaratibu wa kuzuia shughuli za uvuvi wa dagaa katika Ziwa Victoria, mkoani Mwanza, ili kutoa fursa samaki hasa dagaa kuzaliana katika kipindi cha mbalamwezi, hatua ambayo imewaathiri wavuvi kutoka Kenya ambao wanategemea Ziwa Victoria upande wa Tanzania. 

George Ajowi-RFI Kiswahili Miuru Bay

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.