Pata taarifa kuu

DRC: Joto la  kisiasa lapanda kuelekea uchaguzi mkuu wa urais

NAIROBI – Miezi sita kabla ya nchi ya DRC haijafanya uchaguzi wake mkuu, joto la kisiasa kuelekea uchaguzi huo limeendelea kupanda, hali iliyowafanya wanadiplomasia kutoka mataifa 16 ya magharibi kutoa wito wa amani.

Ramani ya DRC
Ramani ya DRC RFI/Anthony Terrade
Matangazo ya kibiashara

Ni kutokana na sintofahamu zinazoanza kushuhudiwa, kumewafanya wanadiplomasia kutoka nchi za umoja wa Ulaya, Canada na Japan, kutoa tamko la pamoja kukemea vitendo vinavyoweza hatarisha ustawi wa demokrasia na amani.

Katika tarifa yao, wanasema nchi zao ziko tayari kuisaidia Congo kufanya uchaguzi wa amani, haki na uwazi, lakini itategemea utayari wa wanasiasa pamoja na Serikali.

Aidha wametaka kuheshimiwa kwa haki za watu kuandamana na kukusanyika bila ubaguzi, wakikashifu matamshi yanayoashiria kuwagawa raia kwa misingi ya kidini, kisiasa na kikabila.

Wanadiplomasia hao wameongeza kuwa, wanaguswa na matukio ya hivi karibuni, ambapo polisi walitumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa upinzani waliojaribu kuandamana jijini Kinshasa.

Kadhalika, mabalozi hao wameonesha wasiwasi na namna tume ya uchaguzi CENI imeshindwa kufanyia kazi mapendekezo ya wadau ikiwemo kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa maandalizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.