Pata taarifa kuu

Kamanda wa kikosi cha EAC nchini DRC arejea Nairobi

Nairobi – Aliyekuwa kamanda wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika mashariki nchini DRC, Meja Jenerali Jeff Nyagah, amekanusha taarifa zilizoenezwa mitandaoni kuwa amejiuzulu baada ya shutuma kuwa ameshindwa kutekeleza wajibu wake katika kurejesha amani mashariki mwa DRC .

Meja Jenerali Alphaxard Muthuri Kiugu ateuliwa kama Mkuu Mpya wa Vikosi vya EAC kule DRC .
Meja Jenerali Alphaxard Muthuri Kiugu ateuliwa kama Mkuu Mpya wa Vikosi vya EAC kule DRC . © Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Barua iliyosambazwa mitandaoni na ambayo pia RFI Kiswahili iliipata nakala, ilisema kuwa Meja  Jenerali Jeff Nyagah Kamanda wa Vikosi vya EAC huko mashariki mwa DRC amejiuzulu kufuatia kile anasema ni tishio kwa usalama wake na juhudi zinazofanywa na  vikosi vya EAC .

Hata hivyo Akizungumza na RFI Kiswahili Nyagah alikanusha ripoti hizo na kusema kwamba anaenda Nairobi kwa mashauriano. 

Kwa mujibu wa barua hiyo, Meja Jenerali Jeff Nyaga anaeleza kuwa kumekuwepo  na vitisho vinavyoeelekezwa katika utendakazi wake, akisema kuwa baadhi ya watu anaodai kuwa mamluki wa kigeni wamekuwa wakituma ndege zisizo na rubani katika makaazi yake haswa mwezi Januari hatua iliyomlazimu kubadilisha makao yake.

Meja generali Jeff Nyagah, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya EACRF nchini DRC
Meja generali Jeff Nyagah, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya EACRF nchini DRC © EACRF

Kando na kile anachodai ni kupokea vitisho katika usalama wake, kiongozi huyo ameongeza kuwa kumekuwepo na kampeni zinazolenga kulichafua jina lake katika mitandao ya kijamii inazofadhiliwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya. 

Aidha ameendelea kusema kuwa utendekazi wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo umekuwa ukikashifiwa, huku baadhi wakidai kuwa vikosi hivyo vimeshindwa majukumu yake na kufanya kazi kwa ushirikiano na waasi wa M23. 

Suala ya kufungwa kwa mtandao wa facebook wa vikosi hivyo likiwa miongoni mwa yale anayosema ni njia moja ya kudhoofisha utendakazi wa nchini DRC. 

Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC
Wanajeshi wa EAC wanaopambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC AP - Ben Curtis

Jenerali Nyaga ameituhumu serikali ya DRC kwa kuchangia katika baadhi ya changamoto ambazo kikosi hicho kinapitia nchini humo, ikiwemo kutowalipa kodi za ofisi za vikosi hivyo, kukosa kuwalipa wafanyikazi katika makao makuu ya vikosi hivyo, kukosa kulipa ada za umeme hatua ambayo ni kinyume na makubaliano yalioafikiwa. 

Wananchi wa Drc pia walikuwepo na maoni kuhusu hatua yake Jeff Nyagah.

00:14

Maoni ya wananchi wa Drc kuhusu Jeff Nyagah

Huku haya yakijiri namna hiyo, taarifa kutoka wizara ya ulinzi nchini Kenya zinasema kuwa Meja Jenerali Alphaxard Muthuri Kiugu ndiye ameteuliwa kuchukua Nafasi ambayo imeachwa na Jenerali Jeff Nyagah kama Mkuu Mpya wa Vikosi vya EAC kule DRC 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.