Pata taarifa kuu

Rwanda: Paul Paul Rusesabagina kuachiwa huru

NAIROBI – Nchini Rwanda, Paul Rusesabagina, mpinzani wa serikali ya Kigali, aliyefungwa jela miaka 25 kwa kosa la ugaidi, ataachiwa huru kesho.

Paul Rusesabagina, mpinzani wa rais Paul Kagame kuachiwa huru
Paul Rusesabagina, mpinzani wa rais Paul Kagame kuachiwa huru © ap
Matangazo ya kibiashara

Hili limebainishwa na afisa wa serikali ya Rwanda. Ripoti zaidi zinasema, Rusesabagina aliyejipatia umaarufu kwa kuwaokoa watu na kuwapa hifadhi katika hoteli aliyokuwa anaifanyia kazi wakati wa mauji ya kimbari mwaka 1994, baada ya kuachiwa anatarajiwa kusafirishwa mjini Doha na baadaye kwenda nchini Marekani.

Aidha, inaelezwa kuwa hatua hii imekuja baada ya Rusesabagina ambaye ana ukaazi wa kudumu nchini Marekani, kumwandikia barua rais Paul Kagame na kuomba msamaha.

Marekani imekuwa ikishinikiza kuachiwa huru kwa Rusesabagina, ambaye wakati wa kesi yake, alikanusha mashtaka dhidi yake na kusema yalikuwa ya kisiasa kwa sababu ya upinzani wake kwa uongozi wa serikali ya Kigali.

Mapema mwezi huu, rais Kagame alisema kulikuwa na mazungumzo kuhusu hatima ya Rusesabagina, ambaye alifungwa jela mwezi Septemba mwaka 2021 na kuahidi kuwa mazungumzo hayo yangeishia, mpinzani wake kusamehewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.