Pata taarifa kuu

Rwanda: Kifungo cha miaka 25 jela dhidi ya mpinzani Paul Rusesabagina 'chapunguzwa'

Nchini Rwanda, kifungo cha miaka 25 dhidi ya Paul Rusesabagina "kimepunguzwa" kwa agizo la rais kulingana na msemaji wa serikali Yolande Makolo. 

Paul Rusesabagina alipata umaarufu kupitia filamu "Hotel Rwanda" ambayo inaelezea jinsi Mhutu huyu mwenye msimamo wa wastani ambaye alikuwa msimamizi wa Hôtel des Mille Collines katika mji mkuu wa Rwanda aliokoa zaidi ya watu 1,000 wakati wa mauaji ya Kimbari ya dhidi ya Watutsi mnamo mwaka 1994.
Paul Rusesabagina alipata umaarufu kupitia filamu "Hotel Rwanda" ambayo inaelezea jinsi Mhutu huyu mwenye msimamo wa wastani ambaye alikuwa msimamizi wa Hôtel des Mille Collines katika mji mkuu wa Rwanda aliokoa zaidi ya watu 1,000 wakati wa mauaji ya Kimbari ya dhidi ya Watutsi mnamo mwaka 1994. AFP Photos/Simon Wohlfahrt
Matangazo ya kibiashara

Wafungwa wengine kumi na tisa waliohukumiwa kwa ugaidi pia wamejikuta hukumu yao ikipunguzwa kulingana na serikali, ikiwa ni pamoja na afisa wa kundi la waasi la FNL, Callixte Nsabimana. Uamuzi uliochukuliwa, kulingana na serikali, baada ya kuzingatia "maombi yao ya msamaha". 

Rais Paul Kagamé alitangaza njia ya kuachiliwa kwa Paul Rusesabagina mwanzoni mwa mwezi Machi, akithibitisha wakati wa mahojiano kwamba kulikuwa na majadiliano juu ya kifungo cha mpinzani huyo.

Mnamo Mei 2022, Washington ilisema "anazuiliwa kinyume cha sheria" na mahakama ya Rwanda.

Habari hii inakuja chini ya wiki mbili baada ya kutangazwa na Rais Paul Kagame kwamba "majadiliano" yalikuwa yanaendelea kuhusu kifungo cha Bw. Rusesabagina.

Wafuasi wa mpinzani huyo wanabaini kwamba kesi yake iligubikwa na makosa mengi. Na familia yake ilisisitiza juu ya hali ya afya ya mtu huyo mwenye umri wa miaka 68.

Mahakama ilidumisha kifungo chake mnamo mwezi Mei 2022, na vile vile wengi wa washtakiwa wenzake 20 walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi 20 gerezani.

Paul Rusesabagina alipata umaarufu kupitia filamu "Hotel Rwanda" ambayo inaelezea jinsi Mhutu huyu mwenye msimamo wa wastani ambaye alikuwa msimamizi wa Hôtel des Mille Collines katika mji mkuu wa Rwanda aliokoa zaidi ya watu 1,000 wakati wa mauaji ya Kimbari ya dhidi ya Watutsi mnamo mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.