Pata taarifa kuu

Rwanda: Tunatafuta suluhu kuhusu Paul Rusesabagina

NAIROBI – Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema nchi yake inaendeleza harakati za kumaliza mvutano wake na Marekani na Mashirika ya kutetea haki za binadamu kuhusu hatima ya mpinzani wake wa kisiasa Paul Rusesabagina, aliyefungwa jela miaka 25 kwa makosa ya ugaidi.  

Paul Kagame, Rais wa  Rwanda.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Bila kutoa maelezo ya kina, rais Kagame ameuambia mkutano wa Kimataifa kuwa, kazi inafanyika kuhusu hatima ya Rusesabagina, ambaye Marekani na watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakishinikiza achiwe huru.  

“Tunapotaka kusonga mbele na kupiga hatua, mara nyingi tumefikia hatua ya kuwasamehe watu wasiostahili msamaha. Hapa nazungumzia watu ambao wamehusika katika mauji ya kimbari, wamejikuta wakiwa huru. Kuna majadiliano na azungilzo kuona namna ya kutatua suala hili bila ya kuingilia kesi hiyo, na naamini kuwa, mwafaka utapatikana.” amesema rais Kagame. 

Rusesabagina alikuwa Meneja katika Hoteli jijini Kigali na alipatia umaarufu wa kuwahifadhi mamia ya raia wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.  

Watetezi wa haki za kibinadamu wamekuwa wakiituhumu Rwanda kwa kwa kumfunga Rusesabagina kwa sababu za kisiasa, madai ambayo Kigali inakanusha. 

Mwezi Agosti mwaka 2022, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, katika ziara yake jijini Kigali, alisema Rusesabagina ambaye ni mkaazi wa nchi hiyo, alitilia shaka kesi dhidi yake kwa kutozingatia haki. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.