Pata taarifa kuu

Burundi: Wanaharakati watano wa haki za binadamu wakamatwa

Wanaharakati watano wa haki za binadamu wanashikiliwa nchini Burundi tangu siku ya Jumanne na idara ya ujasusi, wanne kati yao walikuwa kwenye uwanja wa ndege wakijianda kusafiri kuelekea Uganda, shirika la haki za binadamu Iteka na chanzo cha polisi wameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye mnamo Juni 26, 2020 katika uwanja wa Ingoma huko Gitega.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye mnamo Juni 26, 2020 katika uwanja wa Ingoma huko Gitega. AFP Photos/Tchandrou Nitanga
Matangazo ya kibiashara

Sonia Ndikumasabo, kiongozi Chama cha Wanasheria Wanawake nchini Burundi na makamu wa rais wa zamani wa Tume Huru ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu, ni miongoni mwa wanaharakati waliokamatwa kwenye uwanja wa ndege katika mji mkuu Bujumbura na Idara ya ujasusi (SNR) , amesema kiongozi wa shirika la haki za binadamu la Iteka, Anschaire Nikoyagize.

Prosper Runyange, mwanachama wa shirika llinalotetea Amani na Kuendeleza Haki za Binadamu (APDH), alikamatwa mkoani Ngozi, kaskazini mwa nchi, "baadaye mchana (Jumanne) kwa waranti wa mwendesha mashtaka. Alipelekwa moja kwa moja katika jela ya polisi kabla ya kuhamishiwa hadi makao makuu ya idara ya ujasusi (SNR) mjini Bujumbura" Jumatano asubuhi, Bw. Anschaire amesema, na kuongeza: "hakuna anayejua kwa sasa sababu ya kukamatwa kwa watu hawa wote".

Mamlaka ya Burundi ambayo ilihojiwa kuhusiana na matukio hayo, imejizuia kuongea chochote, lakini habari hii imethibitishwa kwa shirika la habari la AFP na afisa mkuu wa polisi, ambaye hakutaka kutajwa jina lake. "Hii ni mara ya kwanza kwa wanaharakati wengi wa haki za binadamu kukamatwa kwa wakati mmoja", amebaini Anschaire Nikoyagize.

Tangu aingie madarakani mwaka 2020, Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, ambaye alimrithi Pierre Nkurunziza, ambaye alifariki mwaka huo na ambaye alitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma tangu 2005, anajionyesha kati ya dalili za uwazi kwa utawala, ambao bado uko chini ya ushawishi wa "majenerali" wenye nguvu, na udhibiti thabiti wa mamlaka na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshutumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

"Uhasama wa serikali dhidi ya mashirika ya kiraia na vyombo vya habari vya Burundi vilivyokuwa vimestawi wakati huo unaendelea licha ya kuchaguliwa kwa rais mpya mwezi Mei 2020," shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch (HRW) lilisema mapema mwezi Februari.

Burundi, ambayo haina bahari katika eneo la Maziwa Makuu, ndiyo nchi maskini zaidi duniani katika suala la Pato la Taifa kwa kila mtu kulingana na Benki ya Dunia, ambayo inabaini kwamba 75% ya wakazi wake milioni 12 wanaishi chini ya mstari wa kimataifa wa umaskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.