Pata taarifa kuu
MAHOJIANO

E. Ndayishimiye: 'Hatuna hofu ya chochote kuhusiana na haki za Binadamu nchini Burundi'

Pembezoni mwa mkutano wa Francophone hapo jana mjini Djerba nchini Tunisia, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye kwenye mahojiano maalum amezungumza na RFI na France 24. Ndayishimiye ambaye pia ni Mwenyekiti wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, amezungumzia siasa za ndani ya nchi yake na mvutano kati ya DRC na Rwanda.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, wakati wa mahojiano yake na RFI na France 24.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, wakati wa mahojiano yake na RFI na France 24. © RFI/France 24
Matangazo ya kibiashara

Kwanza wanahabari Marc Pellerman (France 24) na Laurent Correau (RFI)  wamemuuliza rais wa Burundi kuhushu mazungumzo ya kisiasa kati ya Rwanda na DRC…… 

Ndayishimiye ajibu

Kwanza, kuhusu mazungmzo kati ya nchi hizo mbili, kuna hatua inayopigwa, kwa kukubali kuketi na kuzungumza ni hatua kubwa, kwa hivyo naona ni maendeleo, kulikuwa na mikutano mingi na nimeona Jumuiya ya Kimataifa inafahamu mchakato huu ili tuwe na amani kwenye ukanda. 

Pellerman na Laurent Correau : Serikali ya DRC iko sahihi kuishtumu Rwanda kuwanga mkono waasi wa M23 , ? 

Ndayishimiye ajibu:  

Mpaka sasa hilo hatujaliamua kwenye ngazi ya Jumuiya, lakini tunaanda kikao na msuluhishi kuhusu mvitano huu, rais wa Angola na baadaye tutachambua na kusema uhalisia wa mambo. 

Mahojiano haya maalum yamepita kwenye Runinga ya France 24 saa 12 na dakika 15 jioni na RFI idhaa ya Afrika yatapita saa 2 na nusu usiku, na tutaendelea kukuletea alichokisema kwenye matangazo yetu ya kesho. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.