Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC

Rwanda yamuua mtu anayeaminiwa kuwa mwanajeshi wa DRC

Jeshi la Rwanda limemuua mtu anayeaminiwa kuwa mwanajeshi kutoka nchi jirani ya DRC, katika Wilaya ya mpakani ya Rubavu, katika kipindi hiki uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukiwa mbaya, kuhusu waasi wa M23.

Wanajeshi wa Rwanda
Wanajeshi wa Rwanda AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyotolewa na jeshi la Rwanda inasema mtu huyo aliyekuwa amevalia magwanda ya jeshi la DRC na ambaye hakutambuliwa mara moja, anaamiwa kuwa mwanajeshi wa FARDC.

Aidha, jeshi la Rwanda linasema mtu huyo alivuka kizuzi cha "Petite Barrière" na kuanza kuwafyatulia risasi maafisa wa usalama, wakati alipopigwa risasi na mwanajeshi wa nchi yake kuepusha madhara zaidi.

Afisa wa DRC ambaye alikuwa katika eneo la tukio na kutotaka kufahamika amesema hakuna mwanajeshi wa DRC aliyekuwa anapiga doria katika eneo hilo la mpaka, licha ya makabiliano ya risasi kusikika usiku kucha.

Tukio hili limetokea baada ya mapema mwezi huu, ndege ya kivita ya DRC kuvuka mpaka wa angaa bila ya idhini na kutua katika uwanja wa ndege wa Rubavu, na kuikasirisha Rwanda.

Katika hatua nyingine,  rais Paul Kagame amewataka waasi wa M23 kuweka silaha nchini na kuondoka katika maeneo ambayo wanadhibiti, baada ya mazungumzo na msuluhishi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Aidha, kwa mujibu wa tarifa kutoka kwenye Ofisi ya Kenyatta, Kagame amekubali, kumsaidia rais huyo wa zamani wa Kenya kwenye juhudi zake za kuwahimiza waasi hao kuacha vita dhidi ya vikosi vya serikali ya DRC, kuelekea awamu nyingine ya mazungumzo ya amani kati ya makundi ya waasi na serikali ya Kinshasa, yaliyopangwa kufanyika jijini Nairobi.

DRC inaishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa 23 madai ambayo inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.