Raia wa Burundi waokolewa nchini Uganda wakisafirishwa kimagendo
Jeshi la polisi nchini Uganda, linasema limefanikiwa kuwaokoa raia 24 kutoka Burundi, wengi wao wakiwa wanawake, ambapo walikuwa wakisafirishwa kimagendo kwa kisingizio cha kutafutiwa kazi nchini humo.
Imechapishwa:
Cheza - 00:47
Polisi imesema raia hao walikamatwa baada ya basi walilokuwa wakitumia kusafiri kutoka kwenye mpaka wa Mtukula kukamatwa katika njia kuu ya Kampala, asubuhi ya hivi leo.
Claire Nabakka ni naibu msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda.
“Kupitia uchunguzi tuliofanya tumebaini raia hawa ishirini na wanne kutoka Burundi waliletwa Uganda kufanya kazi za kawaida.” amesemaClaire Nabakka
Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, yanasema biashara ya binadamu kwenye nchi za ukanda imeanza tena kushamiri, ikihusisha maofisa wa juu serikali na kwenye vyombo vya usalama, ambapo raia wamekuwa wakisafirishwa kwenda kufanya kazi katika nchi za kiarabu.