Pata taarifa kuu
BURUNDI

Burundi: Mwanahabari wa Iwacu aliyekuwa ametoweka, apatikana

Mwandishi wa Gazeti la Iwacu, linalochapishwa nchini Burundi nchini Burundi, Jérémie Misago aliyetoweka tangu siku ya jumamosi hatimaye amepatikana, baada ya maafisa wa polisi nchini humo kuingilia kati. 

Mwandishi wa jarida la Iwacu Jérémie Misago akikabidhiwa kiongozi wake na Msemaji wa Polisi
Mwandishi wa jarida la Iwacu Jérémie Misago akikabidhiwa kiongozi wake na Msemaji wa Polisi © Abbas Mbazumutima
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Burundi, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma ni kuwa Jérémie Misago anayefanyia kazi katika Gazeti hilo la Iwacu nchini Burundi amepatikana tangu Jumatatu.

Taarifa zaidi zinasema, mwanahabari huyo alikwenda kushiriki maombi kwenye maeneo ya milimani ya Magara katika Mkoa wa Rumonge pamoja na wengine, taarifa ambayo pia imechapishwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter wa wizara hiyo.

Aidha, ripoti zingine zinasema kabla ya kupatikana kuna video iliyokuwa imerushwa mitandaoni kutoka kwenye simu yake, kama anavyoeleza mmoja wa waandishi wa Habari wenzake. 

Inaonekana kama alitekwa, sababu ukitizama hiyo Video anaangalia huku na kule amekaa chini, ni kama kuna mtu akimwambia neno la kusema, sio yeye binafsi, inaonekana kama ana matatizo 

Inaelezwa tangu siku ya Jumamosi Simu ya Misago ilikuwa imezimwa, hali ambayo ilizua wasiwasi, Mwandishi wetu wa Bujumbura Abbas Mbazumutima amezungumza na Mmoja wa waandishi wa habari wa gazeti Iwacu, na Kwanza amemwuliza iwapo kuna uhalsia wowote kuhusu sauti iliyosikika kwenye Video hiyo. 

 

Inawezekana kuna mtu ana simu yake akimwambia sema hivi, hatuwezi kosa kutilia shaka,  je? Ni sauti yake ? si sauti yake kama tunavyoizoea, Jeremie ni mtu mwenye kuwa na msimamo, hapa utaona amekaa kwenye nyasi na sehemu isiyojulikana ni wapi. 

Taarifa za hivi punde zinasema Mwandishi wa habari Misago Jérémie sasa amekabishiwa kwa jamaa huku uchunguzi kubaini alikuwa katika mazingira gani, ukiendelea. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.