Pata taarifa kuu
KENYA-MAHAKAMA

Kenya: Polisi aliyemuua Wakili maarufu Willie Kimani ahukumiwa kifo

Mahakama nchini Kenya imemhukumu kifo Fredrick  Leliman, aliyekuwa afisa wa polisi aliyepatikana na hatia ya kuhusika na wakili maarufu wa haki za binadamu Willie Kimani mwezi Juni mwaka 2016.

Maafisa wa polisi waliopatikana na hatia ya kumuua wakili wa haki za binadamu nchini Kenya, Willie Kimani mwaka 2016.
Maafisa wa polisi waliopatikana na hatia ya kumuua wakili wa haki za binadamu nchini Kenya, Willie Kimani mwaka 2016. ibtimes
Matangazo ya kibiashara

Wakili huyo pamoja na mteja wake Josephat Mwenda, na dereva wake wa texi Joseph Muiruri waliouawa na miili yao kupatikana mtoni nje kidogo ya jiji kuu Nairobi, wiki mbili baada ya kutoweka.

Jaji Jessie Lessit, amesema Leliman alibainika kuhusika pakubwa na mpango wa kumteka na kumuua, wakili huyo, katika kesi ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu nchini Kenya.

Mbali na Leliman, ambaye amekuwa mshukiwa mkuu, maafisa wengine wa zamani wa polisi Stephen Cheburet na Peter Ngugi, wamefungwa jela miaka 30 huku  Sylvia Wanjiku akipewa hukumu ya miaka 24.

Wakili Kimani, alikuwa akimtetea Mwendwa mwendesha bodaboda, aliyemtuhumu polisi Leliman, kwa kumpiga risasi bila kosa katika kituo cha ukaguzi mwaka 2015 na hivyo, alikuwa anatafuta haki.

Walitekwa wakati wakitoka Mahakamani katika kaunti ya Machakos.

Hukumu hii imetolewa wakati Polisi nchini Kenya, wakiendelea kukabiliwa na rekodi mbaya ya kutekeleza mauaji ya raia kiholela na kuwateka washukiwa wa makosa mbalimbali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.