Pata taarifa kuu

Uhusiano kati ya DRC na Rwanda: Mkutano wa Doha wafutwa

Mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame uliokuwa ufanyike Januari 23, 2023, mjini Doha, nchini Qatar, ulifutwa siku moja kabla. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa wa wasiwasi hasa tangu kuzuka upya kwa mashambulizi ya waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto), mjini Rubavu, Rwanda, Juni 25, 2021.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto), mjini Rubavu, Rwanda, Juni 25, 2021. © AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Paul Kagame na Felix Tshisekedi walipaswa kukutana Jumatatu hii mjini Doha, Qatar. Lakini, mkutano huo haukufanyika, baada ya kufutwa siku ya Jumapili.

Uhusiano kati ya Kinshasa na Kigali umekuwa wa wasiwasi hasa tangu kuzuka upya kwa mashambulizi ya waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu Kaskazini zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Mkutano haujawahi kutangazwa rasmi

Mkutano huu kati ya marais hawa wawili haujawahi kutangazwa rasmi. Haya ni uvujaji kwenye vyombo vya habari ulioibua uteuzi huu. Uvujaji ulithibitishwa isivyo rasmi na vyanzo kadhaa katika marais mbalimbali wanaohusika.

Kile ambacho kilikuwa kimepatikana kwa upatanishi wa Qatar ni kanuni ya mkutano wa Jumatatu hii kati ya Rais wa Kongo Félix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame. Mkutano ambao ungehudhuriwa, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, rais wa sasa wa jumuiya ya Afrika Mashariki, na Moussa Faki Mahamat, mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika. Pia wangehudhuria mkutano huo: Rais wa Kenya William Ruto, mwezeshaji katika mgogoro huu, Uhuru Kenyatta, na Rais wa Angola João Lourenço.

Mkuu wa diplomasia ya Rwanda alikuwa tayari amewasili Doha

Mkutano huu ulitanguliwa na mazungumzo katika ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje. Hatimaye, ilishindikana Jumapili wakati Moussa Faki Mahamat na mkuu wa diplomasia ya Rwanda, Vincent Biruta, walikuwa tayari wamewasili Doha.

Sababu ya kufutwa kwa mkutano huu ni hatua ya rais wa DRC kukataa kwenda Qatar, lakini sababu zake hazijawekwa wazi. dadlili za kufutwa kwa mkutano hu zilianza kuonekana tangu siku ya Jumamosi jioni kwani vyanzo vya karibu na ofisi ya rais vilisema kuwa safari hii haikuwa kwenye ajenda tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.