Pata taarifa kuu
DRC- MABADILIKO KATIKA AFISI YA RAIS

DRC: Rais Tshisekedi afanya mabadiliko katika ofisi yake

Rais Félix Tshisekedi amefanya mabadiliko katika ofisi yake, na kumfuta kazi Fortunat Biselele, mshauri wake wa kibinafsi aliyekuwa na ushawishi mkubwa katika ikulu ya Kinshasa, huku Serge Tshibangu akithihbitishwa kuendelea kusimamia mchakato wa amani mashariki mwa DRC.

Félix Tshisekedi rais wa DRC
Félix Tshisekedi rais wa DRC © Arsène Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wafanyakazi Ikulu ya Kinshasa wametenguliwa huku wengine walionekana kuwa nguzo ya utawala wake na waaminifu kwake na wenye kufanya kazi kwa ufanisi wakithibitishwa.

Miongoni mwa waliofutwa kazi ni Fortunat Biselele, ambaye alikuwa anabeba mzigo mkubwa wa uhusiano kati ya Kigali na Kinshasa.

Alikuwa kiungo muhimu katika kuyaunganisha mataifa hayo mawili kiuchumi na kiusalama.

Lakini kitumbua kilianza kuingia mchanga wakati waasi wa M23 walipokuwa wakisonga mbele kwenye uwanja wa mapambano huko kaskazini mwa Mkoa wa Kivu hivyo ushawishi wake ukapungua hata baadhi katika ofisi ya rais wakaanza kumshuku na kabla ya kuachishwa kazi alikuwa hahusishwi tena katika mikutano.

Kabla ya kuwekwa kando, Fortunat Biselele alihojiwa mara kadhaa na idara ya ujasusi na hata nyumba yake ilipekuliwa kulingana na duru za usalama.

Nafasi yake imechukuliwa na Kahumbu Mandungu Bula. Wakati huo huo Serge Tshibangu amethibitishwa kuwa mkuu wa ufuatiliaji wa michakato mikuu ya amani na ameteuliwa kuwa Mwakilishi Mkuu wa ufuatiliaji wa mkataba wa Luanda pamoja na mchakato wa Nairobi. 

Wakati huo huo atalazimika kusimamia uhusiano wa kweli  na M23, kupitia wajumbe kutoka Kigali, na pia kusimamia mazungumzo na vikundi vingine vyenye silaha.

Wiki moja kabla ya kauchishwa  kazi alisikika akieleza kupitia mahojiano kwamba rais Tshisekedi alivyomtuma Kigali kwa rais Kagame kuzungumzia maswala ya madini ili kila upande unufaike, swala ambalo wachambuzi wa mambo wanaeleza ndio sababu huenda ametenguliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.