Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Mikutano ya kisiasa yarejelewa tena nchini Tanzania

Mikutano ya kisiasa imerejea tena nchini Tanzania kwa mara ya kwanza  baada ya kuzuia kwa takribani miaka saba kwa amri ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hayati John Magufuli na hivi karibuni, marufuku hayo kuondolewa na rais Samia Suluhu Hassan.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA akiwahotubia wafuasi wa chama hicho jijini Mwanza, Januari 21 2023
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA akiwahotubia wafuasi wa chama hicho jijini Mwanza, Januari 21 2023 © Martin Nyoni
Matangazo ya kibiashara

Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kimefanya mkutano wake wa Kwanza jijini Mwanza siku ya Jumamosi.

Kuanzia mapema asubuhi mamia ya wafuasi wa chama hicho waliibuka kwa shangwe kuhudhuria uzinduzi wa mikutano hiyo, wakisema wamekuwa kufungoni kwa muda mrefu na sasa wanajiona huru kufuhia haki ya kikatiba

“Nimefurahi sana, mikutano hii imerejea, tulikuwa kifungoni,” amesema mmoja wa mfuasi wa chama hicho.

“Nimefarijika sana, hakika sasa tunaanza harakati za kuchukua nchi,” mfuasi mwingine alisema.

Wafuasi wa chama cha CHADEMA wakifuatilia mkutano wa kisiasa uliofanyika Jumamosi, Januari 21 2023 jijini Mwanza.
Wafuasi wa chama cha CHADEMA wakifuatilia mkutano wa kisiasa uliofanyika Jumamosi, Januari 21 2023 jijini Mwanza. © Martin Nyoni

Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Aikaeli Mbowe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kuruhusu mikutano hiyo na kuingia katika mardhiano

“Tuliulizwa sana, lakini maridhiano yamezaa matunda, kulikuwa na wale waliofikiri chama chetu kitakufa, “ Mbowe amewaambia wafuasi wake.

Mkutano huu umefanyika katika mji huo wa Mwanza, ambao viongozi hao wa upinzani walikamatwa mwezi Julai mwaka 2021.

Wafuasi wa CHADEMA wakiwasubiri viongozi wao kusubiri katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Januari 21 2023
Wafuasi wa CHADEMA wakiwasubiri viongozi wao kusubiri katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Januari 21 2023 © Martin Nyoni

Kuondolewa kwa vyama vya upinzani kuwa na mikutano ya siasa, kumesababisha mwanasiasa na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho mwaka 2020 Tundu Lissu, kutangaza kurejea nyumbani Januari 25.

Lissu amekuwa akiishi nchini Ubelgiji, alikokimbilia baada ya kupigwa na risasi na watu wasiojulikana karibu miaka saba iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.