Pata taarifa kuu

Mauaji DRC: Ubelgiji yatoa wito kwa Rwanda 'kusitisha msaada wa aina yoyote' kwa M23

Ubelgiji imeitaka Rwanda 'kusitisha msaada wa aina yoyote' kwa kundi la waasi la M23, ambalo uchunguzi wa awali wa Umoja wa Mataifa unabaini mauaji ya raia wasiopungua 131 mwishoni mwa mwezi wa Novemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Paul Kagame, Rais wa Rwanda katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Juni 25, 2022.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Juni 25, 2022. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Takriban raia 131, wakiwemo wanawake 17 na watoto 12, waliuawa kwa kupigwa risasi au kudungwa visu mwishoni mwa mwezi wa Novemba katika vijiji viwili mashariki mwa DRC, kulingana na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa uliotolewa siku ya Alhamisi, ambao unashutumu kundi la waasi la M23.

"Kundi la waasi la M23 linapawsa kusitisha mara moja uhasama na kujiondoa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake (...) Ubelgiji inaitaka Rwanda kusitisha misaada yote kwa M23 na kuendelea kutumia njia zote ili kuweza kuishawishi irudi tena katika mchakato wa kupokonya silaha wapiganaji na kuwarejesha katika maisha ya kiraia”, mesema diplomasia ya Ubelgiji katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Hili ni jambo la nadra sana kutajwa na nchi ya Ulaya ya Kigali kuunga mkono waasi. Kundi la M23 (March 23 Movement) ni waasi wa zamani wenye silaha ambao wengi wao ni kutoka jamii ya Watutsi ambao walichukua silaha mwishoni mwa mwaka jana na kuteka maeneo kadhaa ya kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.