Pata taarifa kuu

Rwanda yaishutumu jumuiya ya kimataifa kwa 'kuchochea' mgogoro mashariki mwa DRC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda ameishutumu jumuiya ya kimataifa kwa 'kuchochea' mzozo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unaosababishwa na makundi yenye silaha, baada ya Marekani kuitaka Kigali kusitisha uungaji mkono wowote kwa waasi.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Kigali, Agosti 11, 2022.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Kigali, Agosti 11, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Katika wito uliyotolewa na Rais wa Rwanda Paul Kagame siku ya Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken "aliweka wazi kwamba msaada wowote wa nje kwa makundi yenye silaha nchini DRC lazima ukomeshwe, ikiwa ni pamoja na uungaji mkono wa Rwanda kwa kundi la waasi la M23".

Mapigano mashariki mwa DRC kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23, waasi wa zamani wa Kitutsi, yamezidisha mvutano kati ya nchi jirani ya Rwanda, ambayo DRC inaituhumu kuwatia moyo waasi hao. Kigali inakanusha kuhusika.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta alisema kuwa Paul Kagame na Anthony Blinken "walikuwa na mijadala mizuri (...) lakini tofauti zimebaki kwenye uelewa wa tatizo".

Mtazamo mbovu (...) wa jumuiya ya kimataifa unaendelea kuzidisha tatizo hilo", aliongeza mkuu wa diplomasia ya Rwanda.

Mara kwa mara Rwanda imekuwa ikilaumu mgogoro wa mashariki mwa DRC kwa mamlaka mjini Kinshasa na kuishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kufumbia macho uungaji mkono wake kwa FDLR (Democratic Liberation Forces of Rwanda), kuldi la waasi wa Kihutu wa Rwanda, ambao baadhi yao walihusika katika mauaji ya Watutsi ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Ikionyeshwa kama tishio na Kigali, kuwepo na vurugu za wanamgambo hao zilihalalisha uingiliaji kati wa Rwanda katika ardhi ya DRC.

Vincent Biruta alisisitiza kuwa "matatizo ya usalama ya Rwanda lazima yazingatiwe", akibaini kwamba "M23 haipaswi kulinganishwa na Rwanda".

Mkutano wa kilele wa Novemba 23 nchini Angola uliamuru kusitishwa kwa mapigano na kufuatiwa na kuondolewa kwa waasi katika ngome walizoteka katika miezi ya hivi karibuni, lakini hakuna waasi wa M23 hawajatekeleza hili hadi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.