Pata taarifa kuu

Marais wa DRC, Rwanda na Burundi wakubaliana vita kusitishwa Mashariki mwa DRC

Mazungumzo ya amani yaliyofanyika leo mchana jijini Luanda nchini Angola kutatua tofauti za kidiplomasia kati ya DRC na Rwanda lakini pia kujadiliana namna ya kutafuta amani Mashariki mwa DRC, yamemalizika na viongozi wa nchi za DRC, Rwanda na Burundi kukubaliana kuwa mapigano kati ya waasi wa M23 na wajashi wa DRC yasitishwe kufikia siku ya Ijumaa, saa 12 jioni.

Wanajeshi wa jeshi la Kongo wakishika doria katika eneo la Kanyaruchinya ambako walikimblia watu waliotoroka makazi yao kufuatia kusonga mbele kwa waasi wa M23 Novemba 15, 2022.
Wanajeshi wa jeshi la Kongo wakishika doria katika eneo la Kanyaruchinya ambako walikimblia watu waliotoroka makazi yao kufuatia kusonga mbele kwa waasi wa M23 Novemba 15, 2022. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja ya viongozi hao Paul Kagame, Felix Thisekedi, Evariste Ndashimiye na mwenyeji wao Jao Lorenso, mbali na kuafikiana kuhusu usitishwaji wa mapigano hayo; wametaka pande zote kuheshimu makubaliano ya awali ya mazungumzo ya Nairobi na Luanda. 

Marais hao pia wametaka kuendelea kutumwa kwa kikosi cha pamoja cha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mashariki mwa DRC, na waasi wa M23 kuondoka katika miji ambayo wanadhibiti baada ya kuanza kupambana na wanajeheshi wa FARDC. 

Makundi mengine ya waasi kama FDLR-FOCA, RED-TABARA, ADF na megineyo, yametakiwa kuweka silaha chini na kuanza zoezi la kujiisalimisha kwa hiari kwa mujibu wa mazungumzo ya Nairobi kwa usaidizi wa jeshi la MONUSCO na lile la Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Aidha, wamekubaliwa kuwa, mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali ya DRC na makundi ya waasi yarejelewe, huku wakimbizi wakitakiwa kurudi nyumbani. 

Viongozi hao pia wametaka mazungumzo ya kidiplomasia kurejelewa tena na ushirikiano kurudi kama ilivyokuwa ndani ya siku sitini zijazo. 

Jeshi la DRC , lile la Jumuiya ya Afrika Mashariki na MONUSCO, yametakiwa kushirikiana na kufanikisha zoezi la kuwapokonya silaha waasi. 

Mwisho, marais hao wamekubaliana kukutana jijini Bujumbura hivi karibuni, kutathmini utekelezwaji wa mapendekezo yaliyotolewa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.