Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC

Rais Kagame adai Thisekedi anatafuta sababu za kuahirisha uchaguzi wa mwaka ujao

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amemshtumu mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Thisekedi kwa kutafuta sababu za kuahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Disemba  mwaka ujao, kwa kuilaumu nchi yake.

Rais wa Rwanda  Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Kagame, amemshtumu Tshisekedi kwa kutaka kutumia changamoto za kiusalama Mashariki mwa nchi hiyo ambazo anazilaumu kwa Rwanda, ili uchaguzi huo usifanyike, akisema changamoto zinazoshuhudiwa zinaweza kutatuliwa iwapo kiongozi wa nchi hiyo jirani hatapanga kuahirisha uchaguzi.

Aidha, amedai kuwa kiongozi huyo wa DRC hakushinda Uchaguzi wa mwaka 2018.

 “Shida hii inaweza kutatuliwa, iwapo nchi moja inayoelekea kwenye uchaguzi Mkuu mwaka ujao, haitajaribu kuandaa mazingira ya dhahrura ili uchaguzi huo usifanyike, sio kwamba alishinda uchaguzi ule wa kwanza , “ amesema Kagame.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo amesema, ni aibu kwa mataifa mengi ya dunia kushindwa kusuluhisha mzozo wa usalama Mashariki mwa DRC bila ya kupata suluhu kwa kipindi kirefu.

Kuhusu madai kuwa nchi yake imekuwa ikiiba rasilimali za DRC, Kagame amekanusha hilo na kusema hayana msingi wowote.

“Sisi sio wezi, wameendelea kudai kuwa tunaiba rasimali zao,” amesema.

Kagame amesisitiza kuwa waasi wa M 23 sio raia wa Rwanda bali ni Wacongomani, ambao serikali yao imekataa kutekeleza mikataba waliyoafikiana katika miaka ya nyuma.

Kauli hii ya Kagame imekuja wakati huu, mazungumzo ya amani kati ya makundi ya waasi Mashariki mwa DRC na serikali ya DRC, yakiendelea jijini Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.