Pata taarifa kuu
DRC

Mazungumzo ya amani kuhusu Mashariki mwa DRC yaendelea Nairobi

Mazungumzo ya amani kati ya makundi ya waasi, serikali ya DRC na wadau wengine yanaanza   siku ya Jumatano  jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya kufunguliwa siku ya Jumatatu.

Mazungumzo ya amani ya tatu ya DRC, wakati wa ufunguzi Jumatatu, 28 2022
Mazungumzo ya amani ya tatu ya DRC, wakati wa ufunguzi Jumatatu, 28 2022 © East African Community
Matangazo ya kibiashara

Mpatanishi wa mazungumzo hayo yanayofanyika chini ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzungumza na wote wanaoshiriki kwenye mazungumzo hayo.

Kuanza kwa mazungumzo haya, kunakuja baada ya kuwasili kwa wawakilishi wa makundi mengine ya waasi kutoka Ituri na Maniema.

Hata hivyo, kundi la waasi la M23 ambalo wiki iliyopita, liliacha mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, halikualikwa kwenye mazungumzo hayo.

Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anahudhuria mazungumzo hayo.Sikiliza ripoti hii kupata mengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.