Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Miili ya watu 16 yapatikana katika mji wa Kamituga kufuatia mmomonyoko wa udongo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, miili ya watu 16 imepatikana katika mji wa Kamituga, Kilomita 165 Kusini Magharibi mwa mji wa Bukavu jimboni Kivu Kusini, baada ya kutokea kwa mmomonyoko wa udongo, katika eneo hilo linalofahamika kuwa migodi ya dhahabu.

Midogi ya  Kamituga Mashariki mwa DRC
Midogi ya Kamituga Mashariki mwa DRC STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia wanasema janga hili limetokea baada ya mvua kubwa kuunyesha katika mji huo ambao umepata hadhi, miaka michache iliyopita.

Anselme Njungu ni mmoja wa viongozi wa mji huo anathibitisha kupatikana kwa miili hiyo.

Mbele yangu kuna miili 16, tunaendelea kutafuta nyingine. Nyumba zimeenda, vitu vya thamani vimeharibika sana, janga hili limeacha kilio.

Ofisi ya Meya wa mji huo inasema tukio hili limetokea wakati ikishuhudia ukosefu wa chumba cha kuhifadhi maiti na waliopoteza maisha watazikwa siku ya Jumanne jioni, kwa mujibu wa msemaji wake, Baruti.

Tumehesabu miili 16 hadi sasa, watoto 10 na wazazi 6. Kati yao, 15 watazikwa leo. Hapa Kamituga hatuna chumba cha kuhifadhia maiti.

Shirika la kiraia katika mji huo, limesema ujenzi kiholela katika mji huo, kumesababisha kutokea kwa janga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.