Pata taarifa kuu

Wamasai wawasilisha malalamiko dhidi ya "kuwekewa alama" kwa ardhi ya Tanzania

Watu kutoka jamii ya Wamasai wamewasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali ya Tanzania, kupinga uamuzi wa "kuweka alama" ardhi ili kulinda wanyamapori, wakili anayewakilisha jamii hiyo amesema Jumatano.

Kihistoria Tanzania imeruhusu jamii kama Massai kuishi kwenye mbuga za wanyama, ikiwa ni pamoja na Bonde la Ngorongoro, eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO. Lakini idadi ya watu na mifugo yake imeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.
Kihistoria Tanzania imeruhusu jamii kama Massai kuishi kwenye mbuga za wanyama, ikiwa ni pamoja na Bonde la Ngorongoro, eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO. Lakini idadi ya watu na mifugo yake imeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. AFP PHOTO/Carl de Souza
Matangazo ya kibiashara

Wamasai wanaoishi katika wilaya ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania wanaishutumu serikali kwa kutaka kuwahamisha ili waandae maeneo ya utalii na uwindaji katika ukanda huu ambao ni miongoni mwa nchi zenye watalii wengi Afrika Mashariki.

Mamlaka ya Tanzania inakanusha shutuma hizi, ikisema kwamba idadi ya Wamasai inayoongezeka inaathiri wanyama na mimea na kwamba lazima "walinde" eneo la karibu kilomita 1,500 la shughuli za binadamu.

"Kesi hiyo ni muhimu kwa wakazi wa Loliondo," wakili Yonas Masiaya ameliambia shirika la habari la AFP. “Eneo hilo halina malisho kabisa na watu wa eneo hilo wanalitegemea ikiwa ni pamoja na malisho na maji,” amesema na kuongeza kuwa jamii inataka majaji kutengua uamuzi wa serikali.

Malalamiko hayo yaliwasilishwa mwezi Septemba, wiki kadhaa kabla ya uamuzi wa mahakama ya Afrika Mashariki ambayo ilikuwa imewatupilia mbali watu wa jamii ya Wamasai. Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki yenye makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania, walikuwa wametoa uamuzi Septemba 30 kwamba hakuna fidia itakayotolewa kwa watu wa jamii ya Wamasai waliofukuzwa katika ardhi yao.

Askari polisi mmoja aliuawa Juni Mosi mkoani Loliondo wakati wa makabiliano kati ya maafisa wa polisi na Wamasai waliokuwa wakipinga kuwekwa kwa “alama” zinazotenganisha maeneo ya makazi ya watu na wanyama pori. Shirika la kiamataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International lilishutumu mamlaka kwa "kuwafukuza wamasai kwa nguvu kinyume cha sheria".

Kihistoria Tanzania imeruhusu jamii kama Massai kuishi kwenye mbuga za wanyama, ikiwa ni pamoja na Bonde la Ngorongoro, eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO. Lakini idadi ya watu na mifugo yake imeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

Mnamo mwezi Juni, wataalam wa Umoja wa Mataifa walisema "walikuwa na wasiwasi na mipango ya Tanzania ya kuwahamisha Wamasai karibu 150,000 kutoka Ngorongoro na Loliondo bila ridhaa yao".

Mnamo mwaka wa 2009, maelfu ya familia za Wamasai zilihamishwa kutoka Loliondo ili kuruhusu kampuni ya Emirati iliyobobea katika utalii, Otterlo Business Corporation, kupafanya maeneo ya uwindaji . Mkataba huu hatimaye ulifutwa na serikali mnamo 2017, baada ya kukumbwa na tuhuma za ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.