Pata taarifa kuu

Rwanda yakosoa uamuzi wa DRC kumfukuza balozi wake

Mamlaka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zimemfukuza nchini humo balozi wa Rwanda, wakati huu waasa wa M23 inaodai wanasaidiwa na utawala wa Kigali, wakichukua miji kadhaa mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, rais wa Angola, João Lourenço na wa DRC, Félix Tshisekedi hapa wakati walipokutana mjini Luanda, Angola. Julai 6, 2022
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, rais wa Angola, João Lourenço na wa DRC, Félix Tshisekedi hapa wakati walipokutana mjini Luanda, Angola. Julai 6, 2022 AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa Serikali ya Kinshasa, Patrick Muyaya, uamuzi huu umekuja baada ya kikao cha baraza la usalama kilichopitia yanayojiri mashariki mwa nchi hiyo.

Muyaya amesema, kutokana na muendelezo wa nchi ya Rwanda kuwasaidia waasi wa M23, rais wa nchi Felix Tshisekedi, aliridhia pandekezo la wajumbe wa baraza la usalama, kumfukuza balozi Vincent Karega na kumpa saa 48.

Kwenye taarifa yake, Serikali imesema ina ushahidi wa kutosha kuthibitisha uwepo wa wanajeshi wa Rwanda kwenye ardhi ya Congo.

Kutokana na uamuzi huu, serikali ya Kigali, imetoa taarifa kuguswa na uamuzi wa DRC, Rwanda ikisema inashangazwa na hatua ya Kinshasa ambayo imeendelea kuficha maovu yake kwa kutumia kivuli cha waasi wa M23.

Hatua hii inazidisha sintofahamiu zaidi ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili, ambazo kila mmoja anamtuhumu mwingine kwa kujaribu kutatiza usalama wa mwingine, Kigali ikidai DRC inashirikiana na waasi wa FDLR.

Jumuiya ya kimataifa imekashifu hatua ya waasi wa M23 na kuonya mataifa ambayo yanashirikiana na waasi hao, bila kuitaja Rwanda moja kwa moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.