Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya na Expertise France wazindua mpango wa usalama wa baharini wa Go Blue

Expertise France, kwa ushirikiano na shirika Huduma ya Walinzi wa Pwani ya Kenya na kwa usaidizi wa kifedha kutoka Umoja wa Ulaya, umezindua juma hili kipengele cha usalama wa baharini cha mpango wa Go blue katika shughuli ziliozfanyika mjini Mombasa juma hili ambapo mwenzetu Ali Bilali alipata fursa ya kuhuduhuria.

Wavuvi katika pwani ya Kenya wakipewa mafunzo ya namna ya kujiokoa wakati wa ajali
Wavuvi katika pwani ya Kenya wakipewa mafunzo ya namna ya kujiokoa wakati wa ajali © @http://www.goblue.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Shughuli hiyo inahusu kutowa mafunzo kwa wavuvi wa Kenya kutoka vitengo tofauti yv ausimamizi na ufuo kuhusu mbinu za kimsingi za kuokoa maisha na mazingira salama ya kufanyakazi.

Jerome Michelet ni Mkurugenzi wa mradi wa habarini wa Umoja wa Ulaya nchini Kenye Go blue.

Mradi Go Blue ni mradi mkubwa sana wa Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Dola Milioni 25 ambao unagawanyika katika vipengele tofauti, kuna kipengele cha maendeleo ya kiuchumi, kuna kipengele cha usalama baharini na kipengele hiki ndicho kinatuhusu sisi upande wa Expertise France. Mradi huu ulianza miaka miwili iliopita na utaendelea baada ya miaka miwili ijayo jumla miaka 4, kuhakikisha ufanisi wa usalama wa baharini katika pwani yote ya Kenya.

Mbali na kupata ujuzi mpya wa usalama, kila mvuvi alipokea koti la kuokoa maisha na mfuko wa kuzuia maji kwa ajili ya simu yake, ikiwa atahitaji kupiga simu kwa msaada. Mafunzo hayo ni sehemu ya kipengele cha usalama wa baharini cha mradi wa Go Blue, mpango wa pamoja wa kuendeleza ajenda ya Uchumi wa Bluu katika Kaunti sita za pwani ya Kenya. Antony Mbebe ni naibu mtaalamu wa mradi huo Go Blue

Ushirikiano kati ya EU na Serikali ya Kenya kuendeleza Ajenda ya Uchumi wa Blue kupitia Maendeleo ya Pwani.

Chini ya mwavuli wa Uchumi wa Blue, lengo la jumla la mpango huu ni kufungua fursa za ardhi ya bahari katika vituo vya mijini vya pwani kwa ukuaji endelevu, shirikishi na endelevu na athari za ajira, wakati wa kuhifadhi na kutumia mazingira ya pwani na baharini. pamoja na kukuza utawala bora na jumuishi wa baharini. Wanufaika wa mradi wamekiri kupokea vema mradi huo. Abdul Saleh Salim anasema:

tumepata ujuzi ambao tulikuwa hatuujuwi, lakini leo tumepata kuyajua, tumepewa mafunzo tofauti kwa ajili ya kuokoa maisha, watu wengi wamekwisha poteza maisha kutokana na kutokujuwa kwa kweli wametusaidia.

Mipango ya Ufaransa kupitia Expertise France

Usaidizi wa Ufaransa umeenea katika kaunti zote sita na utasaidia Kenya kupata usalama wake wa baharini ili kukuza zaidi uchumi wake wa blue. Hii itajumuisha usaidizi katika maendeleo na utekelezaji wa mkakati wa baharini wa Kenya. Aidha, mradi utaimarisha uwezo wa Huduma ya Walinzi wa Pwani ya Kenya na mashirika mengine ya kitaifa na kikanda yanayohusika na usalama baharini, kwa kukuza utamaduni wa kubadilishana habari na ushirikiano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.