Pata taarifa kuu

Watalii kutoka nchi za kigeni wameanza tena kuitembelea Tanzania

Wakati dunia inaadhimisha siku ya Kimataifa ya Utalii hivi leo, huko nchini  Tanzania, bodi  ya wafanyabiashara wanaowahudumia watalii (TATO) imeandaa  maonesho ya shughuli zao jijini Arusha, kwa lengo la kuimarisha tena sekta ya utalii iliyokuwa imeathiriwa na janga la Uviko-19, wakati huu watalii wakianza tena kurejea wakiwemo wanaozungumza lugha ya Kifaransa.

Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Tanzania.
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Tanzania. ©DeAgostini/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Bodi hii ya wafanyabiashara wanaowahudumia watalii nchini Tanzania (TATO) ilianzisha hafla hii ya maonyesho hapo jana siku ya Jumatatu kama kujitangaza kwa ulimwengu, hatua inayokuja miezi kadhaa baada ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua sinema Royal tour kama ishara ya kuunga mkono sekta iliyoathiriwa na Uviko-19., kamaalivyoeleza  Sirili Mkurugenzi wa bodi hiyo TATO

Baada ya huu mdororo tulipoangalia ilivyoathiri maisha yetu na mapato yetu, ni hapo tukatambua kwamba sekta hii ni muhimu zaidi kwa kiasi hiki lakini tangu mheshimiwa rais aliitengeneza ile filamu ya royal tour tumeanza kupata maombi mengi ya wawekezaji wengi kwenye sekta. 

Uwepo wa watalii kutoka ufaransa, nchini Tanzania unadhihidrisha pia kuwa kuna haja ya kupatikana kwa waongozaji wenye ujuzi wa lugha ya wageni kama Kifaransa lugha muhimu katika sekta ya utalii Tanzania kama alivyobainisha Jean Michel Rousset, Mkurugenzi wa shirika la Alliance francaise Jijini Arusha. 

Kwa mujibu wa TATO ni kuwa watalii wengi kutoka Ufaransa waliitembelea nchi hii, miongoni mwao wafaransa waishio Tanzania, mwaka uliopita watalii hao walifikia 35,000 ndio maana tumeona muhimu wanaowatembeza na kuwalisha yaani mapishi waizungumze lugha ya watalii. 

  Izaak Lawuo, mkaazi wa Arusha, ameeleza namna ambavyo wakaazi wanavyonufaika na utalii na pia Faida za kiuchumi zilizopo. 

 Watu wengi wamenufaika sana inaweza kuwa moja kwa moja au sio moja kwa moja ukichukulia manufaa kwa maana ya mahoteli, usafirishaji kwenye makampuni haya ya Tours.

Utalii nchini Tanzania unazalisha ajira za moja kwa moja 600,000 na ajira nyingine kama milioni moja zisizo za moja kwa moja, ambapo inakadiriwa watalii milioni 1.5 walitembelea nchi ya Tanzania Kabla ya janga la Uviko-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.