Pata taarifa kuu
Tanzia kwenye Muziki

Kifo cha mwimbaji wa Rwanda Yvan Buravan, mshindi wa Tuzo ya Prix decouverte RFI 2018.

Yvan Buravan amefariki akiwa na umri wa miaka 27. Mwanamuziki, mwimbaji mzaliwa wa Rwanda, alikuwa na kazi nzuri na ndefu mbele yake. Alikuwa ameshinda Prix Découvertes RFI mwaka 2018 na kwa hivyo alikuwa sehemu ya familia ya RFI. Amefariki nchini India jana usiku kutokana na saratani ya kongosho.

Yvan Buravan.
Yvan Buravan. Anthony Ravera/RFI
Matangazo ya kibiashara

Amefanya mengi akiwa bado kijana: densi ya watu, kuimba, mashindano ya vipaji vya vijana, akihimizwa na familia yake. Baada ya shule ya upili, alijiandikisha katika Shule ya Muziki ya Kigali, akiwa na uhakika wa njia yake. Wakati huo akiwa na umri wa miaka 20 tu. Kibao chake cha Malaika kilitolewa mwaka uliofuata na kilikuwa na mafanikio ya kweli sio tu nchini Rwanda lakini zaidi, katika nchi jirani. Maonyesho yake yanasifiwa na umma. Katika msimu wa joto wa 2018, aliimba Ubelgiji na kisha Burundi. Ilikuwa mwanzoni mwa kazi yake ambapo alijiunga na familia ya wasanii wa Radio France Internationale. Hivyo anakuwa msanii wa kwanza wa Rwanda kushinda Prix Découvertes tangu kuundwa kwake mwaka wa 1981.

 

Mnamo Aprili, aliendesha tamasha huko Paris na kujitambulisha kwa mashabiki zake wa Ulaya.

 

Kisha ikaja The Love Lab, inayojumuisha nyimbo 17. Albamu yenye mada na maudhui ya mapenzi yenye miguso ya r'n'b na muziki wa kisasa. Ambamo kulikuwemo vibao Oya bora, au Garagaza zinazochezwa sana. Kuna ushirikiano na wasanii wengi kama vile waimbaji Charly & Nina, Gakondo, Victor Rukotana, na Mjomba Austin.

Alipokewa katika studio za RFI, alizungumza juu ya wito wake, juu ya mwanzo wake katika ulimwengu wa kisanii, lakini pia juu ya ahadi zake. Timu zote za RFI ziliweza kuthamini taaluma yake, unyenyekevu wake na zaidi ya yote mapenzi yake ya muziki, iwe ya kitamaduni au ya kisasa.

Kisha ukaja wakati wa albamu ya pili. Aliiandalia  mjini Kigali na baadae akaelekea nchini Uswiden mnamo Februari 2020, katikati ya janga la Uvico-19. Ilibeba jina la Twaje, yenye ladha ya mdundo na sauti za afropop na afrobeat anazounganisha na utamaduni wake wa Rwanda. Kwenye Ye Ayee, tunapata mdundo wa ikinimba wa kaskazini mwa nchi. Kwenye VIP, tunampata kwenye duwa na Ish Kevin, mwakilishi wa kizazi kipya cha rappers wa Rwanda. Pia anashirikiana na DJs wenzake Marnaud na Ritu Joel kwenye Impore, ambao nguvu zao ni sawa na dancehall ya Jamaika.

Tangazo la kifo chake lilisababisha wimbi la hisia kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki wake, jamaa zake wakamimina salam ra rambirambi.

Tangazo la kuthibitisha kifo cha Yvan Buravan
Tangazo la kuthibitisha kifo cha Yvan Buravan © @yvanburavan

 

RFI, na wote waliomfahamu nyuma ya pazia la Prix Découvertes, watamkumbuka kijana mmoja mkarimu sana ambaye alitaka kusaidia kuwapa Wanyarwanda na watazamaji wake wote "maisha bora".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.