Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI 2022

Wakenya wakumbana na changamoto mbalimbali wakati wa kupiga kura

Raia nchini Kenya wameendelea kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao wapya katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vituo vya kupiga kura vikifunguliwa saa kumi na mbili kamili asubuhi Afrika Mashariki.

Mpiga kura, katika kituo cha kupigia kura katika eneo bunge la Mathare  jijini Nairobi, akilitafuta jina lake kabla ya kwenda kupiga kura, Agosti, 09, 2022
Mpiga kura, katika kituo cha kupigia kura katika eneo bunge la Mathare jijini Nairobi, akilitafuta jina lake kabla ya kwenda kupiga kura, Agosti, 09, 2022 © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya raia wamejitokeza katika kituo hiki cha kupiga kura kwenye shule ya msingi ya Kiboro katika eneo bunge la Mathare .Sheinazi kanaiza ni agenti wa chama cha kisiasa katika kituo hiki.

“Milolongo iko sawa, waangalizi wako sawa, usalama uko sawa hakuna changamoto ambao tumekumbana nayo isipokuwa matatizo madogo tu kama vile watu wamekosa kujuwa ni wapi wanapigia kura.” amesema.

 Geofery Shivanda, anayewania kiti cha mwakilishi wadi katika wadi ya Mlango kubwa anatofautiana  na Sheinazi Kanaiza. Upande wa mfumo wa kuwatambua wapiga kura kwa njia ya kieletroniki upo chini, hatujaelewa shida ni nini.” amesema 

Afisa wa Tume ya Uchaguzi IEBC akiangalia taarifa za mpiga kura, Agosti 9, 2022
Afisa wa Tume ya Uchaguzi IEBC akiangalia taarifa za mpiga kura, Agosti 9, 2022 © FMM-RFI

Kilomita 17 kutoka hapa upigaji kura uliendelea katika kituo cha kupiga kura cha shule ya Utawala Academy. Hapa pia baadhi ya changamoto zimeibuka Nimepanga laini japokuwa nikutuma ujumbe wa IEBC sipati majibu kwa hivyo nimekosa kuelewa napanga laini upande upi?amesema mpiga kura mmoja.

“Wakati umepanga laini ukidhani kuwa uko sawa baadae unaambiwa mara unafaa kuangalia mtandaoni ndio ufahamu unafaa kupiga foleni wapi, mara pia majina yamechanganyika.” alisema. “Nimeenda kupiga yangu ndugu vidole vimekataa tu”

Mary Adalo amefika hapa saa kumi na moja na nusu asubuhi: “Ninatarajia amani tupige kura kwa amani tu kwa sababu hata tukipigana jerani wako atasalia tu kuwa jirani wako kura itaisha na sisi tutabaki kuwa hapo hapo”

Vituo vya kupiga vinafungwa saa kumi na mbili kamili Afrika mashariki, zoezi la kuhesabu kura likitarajiwa kuaanza jioni ya leo kulinagana na namna ambavyo matokeo yatakuwa yanatumwa kutoka katika majimbo yote 47.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.