Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI 2022

Uchaguzi nchini Kenya 2022: Baadhi ya wapiga kura waamua kutoshiriki kwenye uchaguzi

Nchini Kenya, sio wapiga kura wote waliojitokeza kupiga kura, huku wale waliojitokeza wakielezea tofauti ya hali ilivyokuwa mwaka huu na uchaguzi wa mwaka wa 2017.

Wapiga kura katika Shule ya Msingi ya Kibera, jijini Nairobi, wakipiga kura, Agosti 09 2022
Wapiga kura katika Shule ya Msingi ya Kibera, jijini Nairobi, wakipiga kura, Agosti 09 2022 © RFI/Laura-Angela Bagnetto
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya Wakenya waliamua kusalia nyumbani na kutoshiriki kwenye uchaguzi huu, wametoa sababu mbalimbali.

Kevin Odoga ni kijana mwenye, umri wa miaka 25, na mkaazi wa mtaa wa Kawangaware jijini Nairobi, licha ya kuwa mpiga kura, aliamua kuendelea na majukumu yake ya kuuza mikeka.

“ Sioni sababu ya kupiga kura kwa sababu siwaamini hawa wanasiasa,” amesema.

Nelson Kamochu yeye, alijiandikisha kama mpiga kura katika Kaunti ya Murang’a lakini hakufanikiwa kwenda kupiga kura.

Sikuwa na nauli ya kwenda, nyumbani kupiga kura, imebidi nibaki ili kufanya kazi, nipate kodi ya kulipa nyumba,” amesema.

 

Mwangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete, akitembelea Shule ya Msingi ya Moi Avenue jijini Nairobi, mojawapo ya kituo cha kupigia kura, Agosti, 9 2022
Mwangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete, akitembelea Shule ya Msingi ya Moi Avenue jijini Nairobi, mojawapo ya kituo cha kupigia kura, Agosti, 9 2022 © FMM-RFI

Kwa wapiga kura waliopiga kura mwaka 2017, wamezungumzia uchaguzi wa mwaka huu.

“Mwaka 2017 mambo yalikuwa tofauti, watu walijitokeza kwa wingi,” mpiga kura mmoja amesema.

“Uchaguzi uliopita, ilikuwa rahisi sana kufahamu jina lako, lilipo lakini uchaguzi huu, imekuwa vigumu sana,” amesema mpiga kura mwingine.

Wale waliopiga kura na wale walioamua kusalia nyumba, sasa wanasubiri matokeo ya uchaguzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.