Pata taarifa kuu
KENYA-ODINGA-SIASA

Siasa nchini Kenya: Safari ya kisiasa ya mgombea urais Raila Odinga

Kuelekea uchaguzi wa Jumanne wiki ijayo, Raila Odinga, mmoja wa wagombea wakuu wa kinyanganyiro cha urais, amejitosa tena kwa mara ya tano kutafuta urais wa nchi hiyo.

Mgombea urais nchini Kenya, Raila Odinga
Mgombea urais nchini Kenya, Raila Odinga © Raila Odinga twitter
Matangazo ya kibiashara

Odinga mwenye umri wa miaka 77, anawania urais kupitia muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja, One Kenya, na iwapo atafanikiwa kuingilia Ikulu atakuwa rais wa kwanza kushika madaraka akiwa na umri mkubwa.

Anaingia katika vitabu vya siasa nchini Kenya, kama kiongozi wa upinzani wa muda mrefu anayeungwa mkono na rais anayeondoka madarakani, Uhuru Kenyatta baada ya wawili hao kupatana baada ya uchaguzi wa mwaka 2017.

Odinga ambaye wafuasi wake, humwita BABA, amekuwa na safari ndefu ya kisiasa, tangu kipindi cha harakati za vyama vingi nchini Kenya miaka ya tisini, na kabla ya hapo, alifungwa jela kwa kwa miaka sita kwa madai ya kushiriki njama ya kutaka kuipindua serikali ya aliyekuwa rais Hayati Daniel Arap Moi mwaka 1982, lakini hakuwahi kupatikana na kosa na baadaye akaikimbia nchi mwaka 1991 baada ya kuachiwa huru.

Aliporejea nchini, aliendeleza harakati za kupigia siasa za vyama vingi na mara ya kwanza kuwania urais, ilikuwa mwaka 1997 na kumaliza wa tatu.

Alijaribu tena mwaka 2007, 2013 na 2017 nq nyakati zote akamaliza wa pili. Hata hivyo, uchaguzi wa mwaka 2007 uliishia kwenye machafuko ya kisiasa, baada ya kudai kuibiwa kura, hali iliyopelekea kuundwa kwa serikali ya muungano ana akahudumu kama Waziri Mkuu.

Wafuasi wake wanamsifia kama kiongowzi mpenda haki na kiongozi anayependa kuongoza mageuzi kwa ajili ya wanyonge lakini wapinzani wake wanamwona kama mwanasiasa, asiyeridhika na anayependa kuihangaisha serikali iliyo madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.