Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Wakili David Mwaure anayetafuta urais nchini Kenya

Nchini kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 9 ya mwezi Agosti, mmoja wa wagombea urais David Mwaure, anaahidi kupambana na rushwa iwapo atashinda uchaguzi huo.

Wakenya wakipiga kura katika Uchaguzi wa mwaka 2013
Wakenya wakipiga kura katika Uchaguzi wa mwaka 2013 www.fix.co.ke
Matangazo ya kibiashara

David Mwaure Waihiga, msomi na wakili wa muda mrefu anayewania urais kupitia chama cha Agano, anaeleza ni kwanini anautafuta urais.  

 “Nataka kupeleka kenya katika kiwango hicho kingine tuwanze kushindana na south korea na Malaysia na Botswana na Finland kwa sababu hata kenya na afrika kwa jumla tunaweza. ”

 Aidha, anaihidi kupiga vita ufisadi swala analosema ni donda sugu nchini kenya.

 “Nitafuatilia ule wizi unaendelea sasa, umekuwepo na unakuja, kashifa ambazo zimetendeka tangu tupate uhuru nataka kuziangazia tena”

Lakini je wakenya wanamfahamu  ?

“Sijamsikia, kwa hivyo hivi sasa ninajuwa mtu amabye anaitwa william ruto ambaye anagombea kupitia UDA na raila odinga wa azimio”

“Simfahamu vile sana hajaweza kujulikana sana alafu pia yeye hajaweka bidii ile ya kufanya kampeni zake kuweza kujitokeza kwa wanachi ile wamjue zaidi. ”

“Mimi nimesikiza bwana david amabye anataka kuwa rais lakini kwa tv tu”

David Waihiga, Georege wajakoyah , waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na naibu wa rais William Ruto ndiyo walioidhinishwa na tume ya uchaguzi kugombea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.