Pata taarifa kuu
DRC-RWANDA

DRC yasema haitakubali jeshi la Rwanda kwenye kikosi cha EAC

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema haitakubali wanajeshi wa Rwanda, kuwa katika kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kinachopendekezwa kusaidia kuleta utulivu Mashariki mwa nchi yake.

Ris wa DRC Félix Tshisekedi
Ris wa DRC Félix Tshisekedi © AP - JUSTIN LANE
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Kinshasa, Patrick Muyaya amesema DRC haitakubali wanajeshi wa Rwanda kujumuishwa kwenye kikao hicho.

Kinshasa inaishtumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi waliouteka mji wa Bunagana wiki hii, madai ambayo Rwanda inakanusha. Kundi la M 23 linasema limeiangusha helikopta ya kijeshi ya FARDC kwa madai kuwa ilivamia ngome zake za Kabindi na Tshengereo.

Msimamo huu wa DRC, kuelekea kikao cha wakuu wa majeshi kutoka nchu za Jumuiya ya Afrika Mashariki watakaokutana kesho jijini Nairobi, kuamua kutumwa kwa kikosi hicho cha pamoja, katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri.

Siku ya Jumatano, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo DRC ni mwanachama mpya, alitoa wito wa kutumwa kwa haraka kwa kikoso cha pamoja, kuleta utulivu Mashariki mwa DRC.

Hata hivyo, watalaam wa masuala ya usalama wanasema mpango wa kutumwa kwa kikosi hicho ni mzuri kwa lengi la kupata amani ili kuwezesha shughuli za biashara kuendelea katika, lakini huenda ukarudishwa nyuma na baadhi ya mataifa ambayo hayasumbuliwi na utovu wa usalama Mashariki mwa DRC kwa sababu ya maslahi mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.