Pata taarifa kuu
DRC-RWANDA

Serikali ya DRC kupambana na unyanyapaa, uhusiano na Rwanda ukiendelea kuyumba

Viongozi wa serikali ya Kinshasa wameamua kupambana na unyanyapaa na msako dhidi ya watu kutoka kabila la kitutsi nchini humo kufuatia uasi ambao kwa silimia kubwa unaundwa na watu kutoka kabila hilo unaoungwa mkono na Rwanda kulingana na serikali umekalia maeneo kadhaa ya mashiriki mwa nchi hiyo kwa mujibu wa Runinga ya Taifa RTNC.

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi. © Arsène Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa maandamano ya kupinga uasi wa M23 Jumatano juma hilo huko Goma Kivu kaskazini, machafuko yalionekana kuwalenga watu wenye asili ya Rwanda kutokana na maumbile yao.

Jumanne Juma hili huko Kisangani, mji muhimu kaskazini-mashariki, luteni kanali wa jeshi la Kongo, mwenye asili ya Rwanda, alifanyiwa ukatili na wakazi wa eneo hilo pamoja na polisi.

Kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano Patrick Muyaya, baraza la Usalama na ulinzi nchini humo limemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na Mkuu wa Polisi kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kuzuia unyanyapaa na msako dhidi ya watu wenye asili ya Rwanda wakati wa maandamano kupinga uasi wa M23.

Waziri huyo wa mawasiliano amesema baraza la Ulinzi lililoongozwa na rais Félix Tshisekedi mbele ya wajumbe kadhaa wa serikali na wakuu wa vyombo vya usalama wameitaka Rwanda kuondoa mara moja wanajeshi wake katika ardhi ya Congo wanaokalia na kujifanya kuwa magaidi wa kundi la M23.

Baraza hilo la usalama wa taifa limeitaka serikali kusitisha makubaliano yote iliofanya na Rwanda.

Siku ya Jumatatu, M23 iliteka mji wa Bunagana, kituo muhimu cha kibiashara kilichoko kwenye mpaka na Uganda. Mamlaka ziliishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi kijeshi wakati wa shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.