Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-EAC

Rais Kenyatta ataka kikosi cha nchi za EAC kutumwa Mashariki mwa DRC

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametoa wito kwa kutumwa kwa kikosi cha ukanda Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kurejesha usalama katika eneo hilo ambalo limeendelea kuhushudia mauaji ya raia. 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Wito huu wa rais Kenyatta unakuja, kufuatia wiki hii kundi la M 23 kuuteka mji wa Bunagana katika mpaka wa DRC na Uganda, baada ya makabiliano makali kati yao na jeshi la FARDC. 

Makabiliano hayo yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao, wengine wakivuka mpaka na kuingia nchini Uganda. 

Kenyatta amesema huu ndio wakati wa kutumwa kwa kikosi cha pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchini DRC ili kuokoa mchakato wa kisiasa unaoendelea kwa ajili ya kupata suluhu ya mzozo wa kiusalama katika taufa hilo la watu Milioni 90. 

Baada ya hivi karibuni kukutana mjini Goma, wakuu wa Majeshi kutoka nchi saba za Jumuiya hiyo wanatarajiwa kukutana tena  siku ya Jumâpili jijini Nairobi, kumalizia mikakati ya kutumwa kwa kikosi hicho cha pamoja katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini. 

Kikosi hicho kinatarajiwa kushirikiana na jeshi la kulinda amani ma Umoja wa Mataifa MONUSCO ili kuyapokonya silaha makundi ya waasi katika êneo hilo. 

Mwezi Aprili, viongozi wa nchi hizo walikutana jijini Nairobi na kukubaliana kuunda kikosi hicho cha pamoja. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.