Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC-MONUSCO

Rwanda yaishtumu MONUSCO kwa kuegemea upande mmoja

Rwanda inalishtumu jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO kwa kuegemea upande wa serikali ya Kinshasa, kuhusu mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Uhusiano kati ya nchi hizo jirani umeendelea kuwa mbaya, kufuatia madai ya DRC kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi wa M 23 ambao sasa wameuteka mji wa Bunagana, unaopakana na Uganda.

Kinshasa, imezuia safari za ndege za Shirika la Rwanda, kufuatia madai hayo, huku Kigali nayo ikiishtumu jirani yake kwa kushambulia ardhi yake na kuwateka wanajeshi wake wawili.

Jumamosi iliyopita, Umoja wa Mataifa ilitaka pande zote, kuacha aina yote ya machafuko na kuongeza kuwa inaunga mkono kila nchi kuwa huru na mipaka yake kuheshimiwa.

"Wakati DRC inaporusha mabomu nchini Rwanda, hili ni suala hatari linalopaswa kukoma mara moja, " amesema msemaji wa Rwanda Yolande Makolo.

Aidha, amesema “ MONUSCO haipaswi kuwa sehemu ya mzozo au kutazama bila kuchukua hatua yoyote,”.

Rwanda imeendelea kukanusha madai kuwa, inawasadia waasi wa M 23 na kueleza kuwa haina sababu ya kuingia masuala ya DRC.

Uhusiano wa nchi hizo mbili ulianza kuwa wa mashaka, baada ya kukimbilia kwa maelfu ya Wahutu kutoka Rwanda na kupewa hifadhi Mashariki mwa DEC baada ya mauaji ya kimbari yam waka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.