Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Tume ya Uchaguzi yasikiliza rufaa za wanasiasa waliokataliwa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Nchini Kenya, Tume ya Uchaguzi inasikiliza rufaa za baadhi ya wanasiasa waliokataliwa, kwa kutofikia vigezo vya kuwania urais, kuelekea uchaguzi wa mwezi wa nane.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wanasiasa hao ni Wakili Ekuru Aukot kutoka chama cha Thirdway Alliance, hapa anaeleza ni kwanini alikata rufaa kwa Tume ya Uchaguzi.

00:39

Ekuru Aukot

“ Chebukati hakufuata sheria na sisi tutampeleka mahakamani tumkumbushe sheria.” amesema Aukot.

Mfanyabiashara Jimi Wanjigi, aliyekuwa na matumaini ya kuwania urais, kupitia chama cha Safina, naye alikataliwa, anaamini alizuiwa kwa sababu za kisiasa.

00:18

Jimmy Wanjigi

“Huu ni utapeli, ni kana kwamba kuna Mwenyekiti mwingine wa Tume ya Uchaguzi," ameongezea Wanjigi.

Wiki moja, iliyopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, alitangaza majina ya wagombea wanne, waliokidhi vigezo vya kikatiba kuwania urais, na hao ni pamoja na Naibu rais William Ruto, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga na Mawakili Profesa Goerge Wajakoya na Wahiga Mwaure.

Rufaa hizo zinatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii, kuamua hatima ya watu 160 waliokataliwa na Tume ya Uchaguzi kuwania nyadhifa mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.