Pata taarifa kuu
KENYA-UKAME

Kenya: Maelfu ya watoto walazimika kuacha shule kufuatia ukame

Ikiwa ni moja ya athari za ukame uliokithiri unaoendelea kuikumba Kenya – na kwa ujumla zaidi katika Afŕika Mashaŕiki – maelfu ya watoto wanalazimika kuacha shule.

Kenya inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika Pembe ya Afrika, na kulazimu familia nyingi za wafugaji kuyahama makazi yaona kwenda mbali zaidi. Hapa, baba anamsaidia mwanawe mwenye utapiamlo kaskazini mwa Kenya, Mei 12, 2022.
Kenya inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika Pembe ya Afrika, na kulazimu familia nyingi za wafugaji kuyahama makazi yaona kwenda mbali zaidi. Hapa, baba anamsaidia mwanawe mwenye utapiamlo kaskazini mwa Kenya, Mei 12, 2022. AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Hivi ndivyo hali ilivyo, kwa mfano, katika Kaunti ya Garissa, kaskazini-mashariki mwa Kenya, ambapo ukosefu wa maji na malisho hulazimisha familia kuhama na kufanya watoto kuacha shule.

Lou Vincent ni naibu mkurugenzi wa shule hii ya Goreyale. Hajawahi kuona idadi ya wanafunzi ikishuka kiasi hiki: “Kabla ya ukame, tulikuwa na wanafunzi zaidi ya 700 na sasa inabadilika-badilika kati ya 450 na 500. Ni familia za wafugaji. Kwa hiyo ikibidi wasafiri mbali sana na mifugo yao kutafuta maji na malisho, wanakwenda na watoto wao. »

Baada ya miezi saba ya kuhamahama, mbali na shule, Aboubakar Ahmed amerejea shuleni hivi punde: “Nilifuata familia yangu, bado huko halikohamia. Ninaishi na jamaa. Nliliacha shule kwa miaka mingi, na nilikosa mtihani lakini ninafanya kinacho wezekana ili niweze kuufanya.

Mnamo mwezi wa Septemba mwaka jana, baada ya miaka mitatu ya ukame tayari, uongozi ulikuwa umeamua kuongeza maradufu kiwango cha chakula kilichotolewa kwa wanafunzi, anaeleza Ahmed Omar, mwalimu mkuu: “Huo ndio mchele wetu. Hapo awali, tulitayarisha kilo 15 kwa siku. Sasa tuna kilo 30. Tunafanya hivi, tukitumaini kuwashikilia watoto shuleni. »

Lakini mwalimu ana hofu kwamba kiwango hiki cha vyakula hakitoshi. Hakuna hata tone la maji ambalo limeanguka kwa miaka miwili huko Goreyale. Na msimu wa mvua unakaribia kumalizika.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masula ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, zaidi ya watu milioni 18 tayari wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula na kuongezeka kwa utapiamlo katika nchi tatu za Pembe ya Afrika, ambazo ni Ethiopia, Kenya na Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.