Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Kenya: Ruto adai kuna njama za kumwibia kura

Mgombea wa urais kupitia muungano wa Kenya Kwanza, Naibu rais William Ruto katika kikao na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, amedai kuwa wapiga kura zaidi ya Milioni Moja hasa kutoka ngome zake wameondolewa kwenye daftari la kupigia kura kuelekea uchaguzi wa mwezi Agosti.

William Ruto, naibu rais wa Kenya anayewania urais kupitia muungano wa Kenya kwanza, akiwa kwenye kampeni za kisiasa Januari 18 2022
William Ruto, naibu rais wa Kenya anayewania urais kupitia muungano wa Kenya kwanza, akiwa kwenye kampeni za kisiasa Januari 18 2022 REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Ruto amewataka Mabalozi hao kuingilia kati suala hili na kuhoji ni vipi majina ya wapiga kura yametoweka ghafla katika daftari hilo.

“Naomba mhoji Tume ya Uchaguzi na maafisa wakuu walio serikalini kuhusu suala hili,” amesema Ruto.

Ruto na washirika wake, katika kipindi hiki cha kampeni, wamekuwa wakidai kuwa, kuna mpango wa kumwibia kura, njama ambazo amesema hazifanikiwa.

“Nyinyi ndio mnapiga kura au mfumo wa serikali” ? aliwauliza wafuasi wake.

Aidha, ameapa kuhakikisha kuwa kura zake, zinalindwa na anaibuka mshindi kwenye uchaguzi huo ambao mshindani wake mkuu ni kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Hii ndio mara ya Kwanza, Ruto mwenye umri wa miaka 55, anawania urais kwa mara ya kwanza baada ya kudumu kama naibu rais tangu mwaka 2013 alipoingia madarakani na rais Uhuru Kenyatta ambaye wametofautiana kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.