Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Kenya: Musyoka arejea Azimio, amuunga mkono Odinga kuwania urais

Nchini Kenya, kiongozi wa chama Wiper, Kalonzo Musyoka, kwa mara nyingine, ametangaza kujiondoa kwenye kinyangayiro cha urais, na kumuunga mkono  mgombea wa muungano wa Azimio Raila Odinga kuelekea Uchaguzi wa mwezi wa nane.

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, akiungana na mgombea wa urais Raila Odinga (Kulia) kwenye mkutano wa kampeni Juni 2 2022 jijini Nairobi
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, akiungana na mgombea wa urais Raila Odinga (Kulia) kwenye mkutano wa kampeni Juni 2 2022 jijini Nairobi © skmusyoka
Matangazo ya kibiashara

Musyoka pia amekubali uteuzi wa Waziri mwenye wadhifa wa juu, iwapo Odinga atashinda uchaguzi na kuunda serikali.

Aidha,amempongeza Martha Karua kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Odinga na kuahidi kumuunga mkono.

“ Nampongeza dadangu Martha na namuunga mkono kwa asilimia zote,” amesema

Awali, Musyoka baada ya kukosa kuteuliwa kama mgombe mwenza wa Odinga, alitangaza azma yake ya kuwania urais, na hata akamtangaza mgombea mwenza wake, na alikuwa amepangiwa kufika mbele ya Tume ya Uchaguzi siku ya Jumamosi.

Baada ya kutangaza kumuunga tena Odinga, wote waliungana katika mkutano wa kampeni jijini Nairobi na kuahidi kumfanyia Odinga, kuhakikisha kuwa anaingia madarakani.

“Mimi ndio Messi waz Azimio, nilikuwa nimepumzika sasa, nimerejea,” alisema huku akishangiliwa na wafuasi wake.

Odinga naye amempongeza, Musyoka kwa kurejea na kusema sasa kikosi cha muungano wake wa siasa kimemalizika.

“Kikosi chetu sasa kimekamilika, Kalonzo Musyoka, anashikilia nafasi ya 11, “ alisema Odinga.

Muungano wa Azimio la Umoja, sasa unatarajiwa kuzundua ruwaza / Ilani yake Jumatatu, wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.