Pata taarifa kuu
Rwanda Haki

Rwanda : Marekani yakosoa kufungwa kwa Rusesabagina

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema uchunguzi wake umebaini kuwa, muigizaji wa filamu ya Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina, ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauwaji ya kimbari nchini Rwanda, alifungwa jela kimakosa nchini Rwanda.

Paul Rusesabagina shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda
Paul Rusesabagina shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara hiyo amesema hatua ya Marekani imetokana na namna Rusesabigina alivyokamatwa na kwamba kesi yake haikuendeshwa kwa uhuru na haki.

Rusesabagina anatumikia kifungo cha miaka 25 jela, baada ya mahakama ya Kigali kumpata na hatia ya kuhusika na vitendo vya kigaidi.

Hatua ya Rusesabagina kuwaokoa Zaidi ya watu 1,200 wakati wa mauwaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994, ndio ilichangia kuigizwa kwa filamu ya Hotel Rwanda.

Familia ya Rusesabagina mwenye miaka 67, inasema hali yake ya afya inazidi kuwa mbaya, huku ikitaka mataifa ya Marekani na mengine kushinikiza serikali ya Rwanda kumuachilia huru.

Familia hiyo imekuwa ikidai kuwa Rusesabagina alihadaiwa na serikali ya Rwanda kwa kutumia mawakala wake kuondoka Texas Marekani alikokimbilia na kurejeshwa Rwanda

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.