Pata taarifa kuu
Rwanda - Haki

Rwanda : Awamu ya kwanza ya wahamiaji kutoka Uingereza kuwasili hivi karibuni

Waziri mkuu wa Rwanda, Edouard Ngirente, amesema awamu ya kwanza ya wahamiaji kutoka nchini Uingereza, watawasili nchini Rwanda hivi karibuni, na kwamba Rwanda imekamilisha matayarisho ya kuwapokea.

Rais wa Rwanda Paul Kagame na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Rais wa Rwanda Paul Kagame na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson AP - Eddie Mulholland
Matangazo ya kibiashara

Ngirente amesisitiza kuwa mpango huo kati ya  Rwanda na Uingereza una malengo mazuri huku akiwapuuza wanaokosoa mpango huo ambao utagharimu dolla millioni 120, huku baadhi ya watafuta hifadhi wakitarajiwa kusafirishwa hadi taifa la Jamhuri ya Africa ya Kati.

Mashirika ya kiraia yatuhumu hatua hiyo ya serikali ya Rwanda na kuitaja kuwa isyofaa na kukikuka mkubwa wa haki za biandamu, ila Ngirente amesema masharika hayo yatapongeza mpango huo pindi baada ya kutekelezwa vikamilifu.

Tayari waziri mkuu wa Uingereza Boris John, amesema wahamiaji zaidi ya 50, wamepewa taarifa kuwa watakuwa miongoni mwa kundi la kwanza litakalosafirishwa hadi nchi Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.