Pata taarifa kuu

Baadhi ya wahamiaji haramu wanaotarajiwa kwenda Rwanda watoroka.

Mashirika ya kutoa misaada ya binadamu yanasema, wahamiaji kadhaa  haramu walio nchini Uingereza, wanaotarajiwa kusafirishwa nchini Rwanda, wamejificha. 

Rais wa Rwanda  Paul Kagame na waziri mkuu wa Uingereza  Boris Johnson
Rais wa Rwanda Paul Kagame na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson AP - Eddie Mulholland
Matangazo ya kibiashara

Shirika la msalaba mwekundu linasema, baada ya Uingereza mwezi uliopita kutangaza kuwa, wahamiaji haramu, walio katika nchi hiyo, watapelekwa nchini Rwanda baadhi yao wameamua kujificha. 

Aidha, inaelezwa kuwa, wengine wameenda mbali zaidi na hata kutaka kujitoa uhai, kuonesha kupinga mpango huo. 

Mashirika hayo ya kibinadamu, wanaharakati wa haki za binadamu wameshtumu hatua hiyo ya Uingereza ambayo wanasema ni kinyume cha haki za binadamu. 

Uingereza imesema kundi la kwanza la wahamiaji,watataarifiwa  hivi karibuni kuhusu kuanza  mpango wa serikali ya kuwahamisha kwenda nchi ya Rwanda ambayo imesema iko tayari kuwapokea kwa mujibu wa mkataba uliotiwa saini kati yake na Uingereza. 

Makubaliano hayo ya ubadilishanaji wa wahamiaji haramu  kati ya Rwanda na Uingereza yalipingwa vikali na baadhi ya raia nchini Uingereza wakisema kuwa serikali imeshindwa kuwajibika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.